TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 5 October 2014

TUNAENDELEA KUMSHUHUDIA YESU KRISTO AKIFUNGUA WATU KUTOKA KWENYE VIFUNGO MBALIMBALI.

Hakika Bwana wetu Yesu Kristo ananendelea kutenda miujiza mpaka sasa, Dada Julieth John alifika katika ibada ya Jumapili hapa Life in Christ Ministries Zoe akiwa na maumivu ya miguu yaliyomsumbua kwa muda sasa, lakini wakati wa  maombi ya kufunguliwa kwa pamoja (Mass Prayer au Mass deliverance) maombi yaliyoongozwa na Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph, dada Julieth aliweza kupokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.


                          Hapa dada yetu akiwa amekaa na akionekana ni mwenye maumivu.
                                                    Akimshukuru Mungu kwa kumponya.



Kutokana na maumivu aliyokuwa nayo ya mguu hakuweza kukimbia lakini hapa tunaona baada ya maombi aliweza kukimbia.

Yote yanawezekana kwake yeye aaminiye. Utukufu ni kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


Hakika Mungu anashangaza sana kwa nguvu zake na miujiza yake,Mama Oliver alikuja akiwa na maumivu ya kiuno na mguu lakini naye alipokea uponyaji wake kupitia Mass Deliverance.


                          Hapa akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo.
                          Hapa akichuchumaa bila ya kuwa na maumivu ya aina yoyote.














No comments:

Post a Comment