Mama Elizabeth Joseph
alifika katika nyumba ya Mungu Life in Christ Ministries Zoe akisumbuliwa na
tatizo la mifupa, tatizo hilo lilisababisha ashindwe kutembea vyema lakini pia
hakuweza kukunja miguu yake na pia alikuwa na maumivu makali katika miguu yake
na katika mgongo wake.
Alikwenda hospitali
vipimo vikaonyesha sehemu ya mifupa yake ilikuwa ikisagika ndipo alipoamua
kufika katika nyumba ya Mungu ili aweze kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo
wa Nazareth, hakika yanayoshindikana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana.
Ulifika wakati wa Yesu Kristo kumponya kupitia mtumishi wake prophet Joseph,
wakati wa ibada ya kufunguliwa kwa pamoja mtumishi wa Mungu pophet Joseph
aliamuru kila aliye mgonjwa aweze kupokea uponyaji ndipo ndugu yetu Elizabeth
Joseph aliweza kupokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.
Alisimama papo hapo na kuanza kutembea hii ni ikiwa mara ya kwanza kutembea
bila ya kushikiliwa baada ya kukaa muda mrefu ya bila kutembea sawasawa.
Mume
wake alistaajabu kuona jambo ambalo Mungu amemtendea mkewe alikwenda kwenye
madhabahu kushuhudia matendo makuu ya Mungu. Dada Elizabeth akiwa anaingia kwenye nyumba ya Mungu L.C.M Zoe.
Akiwa kwenye nyumba ya Mungu tayari kwa kupokea uponyaji wake.
Hapa akisaidiwa kusimama na mtenda kazi katika ya nyumba ya Mungu.
Akitembea mwenyewe bila ya msaada wa mtu yeyote hii ni baada ya maombi.
Akishuhudia matendo makuu ya Mungu.
Mume akimshukuru Mungu kwa uponyaji wa mke wake.
Akitembea bila ya tatizo lolote.
Yanayoshindikana kwa madaktari kwa Yesu Kristo wa Nazareth yanawezekana. Utukufu kwa Mungu.
No comments:
Post a Comment