TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Wednesday, 2 September 2015

KANSA NA FIBROID YAKOMA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Julieth Ngemela aliletwa kwenye nyumba ya Mungu akiwa mdhaifu sana kutokana na kusumbuliwa na tatizo la kansa lakini mbali na kusumbuliwa na kansa pia alikuwa akisumbuliwa na uvimbe kwenye tumbo (fibroid). Kutokana na uonevu wote huo wa ibilisi hakuweza kutembea wala kukaa aliletwa kwenye nyumba ya Mungu L.C.M Zoe na kulazwa kwenye machela kutokana na kushindwa kukaa.

Wakati wake wa kupokea uponyaji kutoka kwa mtenda miujiza Yesu Kristo wa Nazareth ulifika, wakati wa kipindi cha mstari wa uponyaji kilipofika mtumishi wa Mungu prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu alimwekea mkono na papo hapo ndugu Julieth alipokea uponyaji na akaweza kusimama na kutembea kuonyesha kuwa hakika Yesu Kristo wa Nazareth amemponya moja kwa moja na ndio ukawa mwisho wa kansa kumtesa.

                         Ndugu Julieth Ngemela akiwa amejipumzisha kwenye mkeka.

               Akiwa amebebwa kwenye machela tayari kuwekwa kwenye mstari wa uponyaji.
                           Akiwa amewekwa kwenye machela katika mstari wa uponyaji.



                        Prophet Joseph akiamuru roho zote za maumivu kumwacha.
                                Akiamuru udhaifu katika miguu kumwacha.
                                      Prophet Joseph akimwamuru kusimama na kutembea.
                     Mara baada ya maombi alisimama na kutembea mwenyewe bila ya kubebwa.
                                                       Akimshukuru Mungu kwa kumponya.

No comments:

Post a Comment