Hakuna kifungo ambacho Yesu hawezi kukifungua wala hakuna ngome Yesu asiyoweza kuivunja. Kaka David alikuwa kwenye kifungo cha ulevi wa bia ya Castle light kwa muda mrefu ndipo alipoamua kwamba lazima ulevi huu ufikie mwisho wake lakini si kwa nguvu zake maana kwa nguvu zake alikwisha shindwa kuacha ndipo alipoamua kutafuta mahali ambapo Yesu mtenda miujiza atamfungua, alifika kwenye huduma ya LIFE IN CHRIST MINISTRIES ZOE,na Yesu hakumpita alimfungua naye akawa huru kweli kweli. Kama anavyoonekana kwenye picha. Alikuja na pombe hii ili kuonyesha kwamba ni kweli amekuwa akiitumia pombe hii.
|
Kaka David akielezea huku akiwa ameshikilia pombe hiyo mkononi. |
Prophet Of God Prophet Joseph akimuombea ili kuondoa kiu yote ya pombe iliyomtesa kwa miaka mingi.
Kaka Richard naye alifika ili akutane na Yesu atakayemtoa katika kifungo cha kula ugoro, na kunywa viroba kwa miaka mingi.
Hapa akieleza jinsi ambavyo amechoka kuteseka na kifungo cha ulevi.
Akionyesha jinsi anavyokula ugoro.
Hapa akionyesha jinsi ambavyo hunywa kiroba
Prophet Joseph akimfungua kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Baada ya kufunguliwa alipojaribu kuonja hakuweza kumeza kwasababu ile roho chafu ya ulevi ilikuwa imekwisha ondolewa na Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment