Janeth Mkwawa alipata ajali jumatatu iliyopita, aliteleza akiwa nyumbani kwake na kutegua mguu wake na kusababisha sehemu ya mfupa kuwa nje kutokana na mguu huo kupasuka. Alikwenda hopsitalini na kushonwa nyuzi saba alifika katika nyumba ya Mungu Zoe akiwa hajiwezi alikuwa akitembea kwa shida na maumivu makali, alipokea uponyaji baada ya mtumishi wa Mungu Prophet Joseph kuamuru roho chafu za magonjwa kuwaacha watu kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth. Ndipo alifika mbele kutoa ushuhuda mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akasema dada Janet anahitaji kuwekwa huru tena kwasababu anachikiona ni kuwa mpango wa ibilisi ni kusababisha dada Janeth arudi hospitali tena na takaporudi kufanyiwa operasheni ibilisi atamtega na kusababisha madaktari kumkata mguu huo, wakati akiamuru kila roho chafu kumwacha dada huyu roho chafu zikakiri kuwa ni kweli ndio mpango wao ambao wameupanga kwa dada huyu lakini kwakuwa hakuna nguvu inayoweza kushindana na nguvu ya Mungu dada huyu aliwekwa huru kutoka katika mtego huo wa ibilisi.
Akishuhudia jinsi Mungu alivyomponya.
Mguu huo ulivyokuwa.
Akitembea bila ya kuwa na maumivu yoyote.
Akimshangilia Mungu kwa kumweka huru kutoka katika mitego ya ibilisi.
Mwana wa Mungu akikuweka huru unakuwa huru kweli kweli.
No comments:
Post a Comment