Mama Agness akiwa anaingia hapa Life in Christ Ministries Zoe,katika eneo la mapokezi.
Mwinjilisti Joyce akimuhoji mama Agness.
Hapa tunaona mama huyu akichukuliwa na nguvu ya Mungu.
Akiwa chini baada ya nguvu ya Mungu kumchukua,nguvu ambayo hufungua,huvunja kila aina ya nira.
Akitoa ushuhuda baada ya kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.
Baada ya maombi aliweza kuunyosha mkono wake,kabla ya maombi hakuweza kuunyosha.
Nesi kutoka kitengo cha mifupa,MOI, Mrs.Sophia Wellya akithibitisha kuwa ni kweli mfupa umeunga.
Nesi akimchukua mama huyu ili akakate hogo.
Hogo likiwa limeondolewa ishara ya kwamba mama huyu haihitaji tena hogo hili.
Hogo likiwa limetupwa chini halihitajiki tena katika mkono wa mama huyu kwa jina la Yesu Kristo.
Mama huyu akilitundika hogo hili kwenye ukuta wa uponyaji hii ikimaanisha kuwa yeye ni mzima na hatalivaa tena hogo hili. Yesu Kristo wa Nazareth anaunga mifupa hata sasa.
No comments:
Post a Comment