Obute Obunya alifika katika huduma ya LCM Zoe akiwa na maumivu katika mkono wake wa kushoto kutokana na mkono wake kuvunjika na kusababisha mifupa kupishana, alifika akiwa na hogo mkononi mwake. Wakati mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph alipokuwa akikemea kila roho za maumivu kuwaacha watu ndugu Obute alipokea uponyaji wake, kutokana na maumivu hayo hakuweza kuendesha gari lake, kupiga makofi wala kunyosha mkono huo juu, kwa neema ya Mungu alipopokea uponyaji wake aliweza kuendesha gari yake na kunyosha mkono wake juu. Afisa muuguzi kutoka katika hospitali ya Taifa ya Temeke alithibitisha kwa kusoma X- ray ya ndugu Obute na kuonyesha kuwa mfupa ulikuwa umepishana na kwa neema ya Mungu mfupa uliunga mara moja.
Mkono unavyoonekana ukiwa na hogo.
Mara baada ya maombi aliweza kuunyosha mkono wake.
Akishuhudia matendo makuu ya Mungu aliyomtendea.
Aliweza kupiga makofi kwa mara ya kwanza mara baada ya kupokea uponyaji.
Afisa muuguzi akikagua mkono huo.
Kamba iliyokuwa imeshikilia hogo ikiwa chini mara tu baada ya mfupa kuunga.
Mke wa ndugu Obute akimshukuru Mungu kwa kumponya mumewe.
X- ray ya ndugu Obute.
Akiendesha gari ambalo mwanzo hakuweza kutokana na maumivu aliyokuwa nayo.
Akiingia huku akiendesha gari kuonyesha kuwa hakika Mungu ameunga mfupa wake.
No comments:
Post a Comment