Peter Mazengo alikuwa akisumbuliwa na fangasi ya ubongo, fangasi hiyo ilipelekea kuhangaika katika hospitali lakini hakupata uponyaji ndipo alipoamua kuamini katika jina kuu lipitalo majina yote, jina la Yesu Kristo wa Nazareth alifika katika nyumba ya Mungu LCM ZOE akitokea hospitali, ambapo alifika akiwa anabebwa na familia yake kutokana na kutokuweza kutembea wala kusimama. Hakika Mungu ni mwema sana kama alivyoamini ndivyo alipokea, ndugu Peter alipokea uponyaji wake na akawa mzima kabisa.
Hivi ndivyo hali ya Ndg. Peter ilivyokuwa.
Hapa akionekana na plasta mkononi kutokana na kuwekewa dripu.
Baada ya kupokea uponyaji nguvu iliingia na akaweza kusimama na kutembea mwenyewe.
Akiwa mbele ya maelfu kushuhudia yale ambayo Mungu amemtendea.
Familia ya ndugu Peter wakimshukuru Mungu kwa kumponya ndugu yao.
Akienda kukaa akiwa ni mwenye nguvu kabisa.
Hakika Mungu wetu anaweza.
No comments:
Post a Comment