Kissa Brown alikuwa na tatizo la kutokwa na damu nzito na nyingi wakati wa udada (hedhi) mpaka ikapelekea kuishiwa damu mara kwa mara alikwenda hospitali akaanza kutumia dawa ili kkuongeza damu lakini haikumsaidia, tatizo hili liliendelea mpaka ikafikia hatua ya kutokuweza kusimama wala kukaa kutokana na kupatwa na kizunguzungu. Mungu ni mwema sana alipofika katika nyumba ya Mungu LCM ZOE kwa neno la msamaha tu dada Kissa alipokea uponyaji wake palepale na mtumishi wa Mungu prophet Joseph aliamuru damu hiyo kuacha kutoka hakika neno la prophet ni neno lenye nguvu damu ilikoma mara ile ile.
Zab 103:3- biblia inasema ; akusamehe na maovu yako yote, akuponya na magonjwa yako yote.
Neno la Mungu ni kweli na hakika.
Dada Kissa akiwa amejilaza chini kutokana na udhaifu aliokuwa nao.
Mara baada ya maombi akiwa na nguvu aliweza kusimama na kushuhudia matendo makuu ya Mungu.
Akielekea chooni kwenda kujikagua jinsi damu ilivyokoma kama prophet Joseph alivyonena.
UTUKUFU KWA MUNGU.
No comments:
Post a Comment