TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Thursday, 19 March 2015

MATENDO MAKUU YA MUNGU YANAENDELEA KUTUSHANGAZA

Hakika Mungu wetu ameendelea kutushangaza kwa matendo yake makuu anayoyatenda, dada Happy Marko kutoka Mkuranga alifika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe akiwa hajiwezi kabisa kutokana na kupooza mwili hakuweza hata kutingisha mikono wala vidole vyake. Wakati mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alipokuwa akikemea roho zote za kupooza dada Happy alikuwa amebebwa  na wainjilisti akielekea maliwato (chooni) ndipo nguvu kutoka juu ilimshukia na kufukuza roho zote za kupooza na ghafla alisimama mwenyewe kwa miguu yake bila ya kushikiliwa na mtu yoyote. Happy alipokea uponyaji huo kutoka Mbinguni kwa baba bila hata ya kuwekewa mkono lakini aliamini kuwa Yesu Kristo anaponya na yeye atapokea uzima na ndivyo ilivyokuwa kwake.


              Dada Happy akiingia kwenye nyumba ya Mungu huku akiwa amebebwa .
                                           Akiwa ndani ya nyumba ya Mungu.
                  Mara baada ya maombi akiwa amesimama bila ya kushikiliwa wala kubebwa.

           Mmoja kati ya wainjilisti waliokuwa wakimbeba akishuhudia na kumtukuza Mungu.
                              Akishuhudia na kumshukuru Mungu kwa kumponya.
                          Ndugu wa dada Happy wakimshukuru Mungu kwa kumponya ndugu yao.
                              Mtoto wa dada Happy akibubujikwa machozi ya furaha.
 Akinyanyuka mara baada ya ugonjwa wa kupooza kumwacha na kuwa huru kama anavyoonekana.
Akiwa amesimama vizuri maana ugonjwa wa kupooza sio sehemu ya maisha yake na Yesu Kristo akiwa amemuweka huru moja kwa moja.

                                            Utukufu kwa Yesu Kristo.





No comments:

Post a Comment