Mwanamziki wa bongo fleva Joseph Haule au kwa jina la kisanii Professor Jay akimshukuru Mungu kwa kumtoa katika roho ya ulevi na pia anamshukuru Mungu sana kwa maana alikuja katika huduma hii ya Life in Christ Ministries Zoe akiwa na maumivu ya miguu lakini Mungu alimponya kabisa na alisema ana kila sababu ya kuendelea kumshukuru Mungu kwasababu amekuwa kwenye sanaa kwa muda usiopungua miaka 20 lakini hakuwa na mafanikio kama aliyonayo sasa baada ya kumpokea Yesu Kristo wa Nazareth.
Hapa Professor Jay akiwa katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe.
Professor Jay akishuhudia maelfu ya waliofika katika huduma ya LCM jinsi ambavyo Mungu amemtendea.
Professor Jay akimwimbia Mungu katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe... Hakika sanaa bila Mungu haiwezekani.Utukufu na sifa kwa Mungu mwenye uwezo wote.
No comments:
Post a Comment