Ndugu hawa waliweza kupokea uponyaji wao baada ya Prophet Joseph kusoma neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Zaburi 107:20, "Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao". Pindi neno hili liliposomwa watu walipokea uponyaji wao na kufunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali. Hawa ni baadhi ya maelfu waliofika katika huduma ya LIFE IN CHRIST MINISTRIES ZOE na kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth akimtumia mtumishi wake Prophet Joseph.
Dada Joyce kutokea Mwanza alikuja akiwa na maumivu ya mgongo baada ya kusoma neno hilo alipokea uzima hapo hapo,hapa akimshukuru Mungu kwa kumponya.
Dada Joyce akiwa ameinama kuonyesha kwamba hana tena maumivu ya mgongo.
Dada yetu Amina kutoka Rufiji alikuja akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo na pia alikuwa hawezi kukaa kwenye mkusanyiko wa watu wengi kutokana na ugonjwa huo lakini baada ya kusoma neno hilo la Mungu alipokea uponyaji wake mara moja.
Yanayoshindikana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana .
No comments:
Post a Comment