Mungu ni mwenye upendo na rehema sana kwetu dada Neema Mbajo alikuwa katika mateso ya muda mrefu kuanzia akiwa katika kidato cha tatu alikuwa akiota anafanya mapenzi na mwanaume asiyemfahamu, ikafikia hatua akawa akimuona mwanaume huyo kinadharia, yaani mwanaume huyo alikuwa akimtokea bila ya kuota. Siku moja akiwa anatembea njiani ndege wawili walikuja na kutua kichwani kwake na kuanza kupigana mara akaanguka na kuzimia alikwenda sehemu nyingi lakini hakupata msaada. Alipomaliza shule aliolewa lakini kutokana na kuwa na mume wa kipepo ndoa yake iliharibika. Pia alijaribu kufungua biashara mbalimbali lakini hazikufanikiwa kutokana na mume huyu wa kipepo kumuharibia biashara na maisha yake. Alipofika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe, Yesu Kristo mtenda miujiza alimfungua kwa kupitia mtumishi wake Prophet Joseph na kuwa huru kabisa kutoka katika mateso ya muda mrefu.
Akielezea jinsi roho hiyo chafu ilivyomtesa.
Hakuna jambo gumu la kumshinda Yesu, yeye ni Alfa na Omega ( ni mwanzo tena mwisho) Utukufu kwa Yesu Kristo.
No comments:
Post a Comment