Dada Febronia akishuhudia matendo makuu ya Mungu.
Miwani ikiwa chini kuonyesha ishara ya kuwa ni mzima kwa jina la Yesu Kristo.
Akiiweka kwenye ukuta wa uponyaji ikiwa na maana haihitaji tena kuvaa miwani.
2. Febronia Temanyika alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kichwa kwa zaidi ya miaka 20 na ilimpelekea avae miwani na pia hakuweza kutembea kwenye jua kali mtumishi wa Mungu,Prophet Joseph alipoamuru maumivu yote ya kichwa kuwaacha watu dafa Febronia alipokea uponyaji wake hapo hapo na kuwa mazima kabisa. Jina la Bwana litukuzwe.
3. Mama Renatha alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mabega na mkono wake ulikuwa unapata ganzi na hakuweza kunyosha mkono huo,baada ya maombi ya Mass Prayer alipokea uponyaji na kuwa mzima kabisa. Pia alipata neema ya kupata shilingi laki moja 100,000/= pesa taslimu kutoka kwa mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph.
Akishuhudia jinsi ambavyo amepokea uponyaji wake.
Prophet Joseph akiwa na mama Renatha.
Mwinjilishi Andrew akimkabidhi mama Renatha pesa hizo.
Prophet Joseph akimshukuru Mama Renatha kwa kupokea pesa hizo .
UTUKUFU KWA BWANA WETU YESU KRISTO.
No comments:
Post a Comment