Dada Brenda kutokea Tabata jijini Dar es salaam ana kila sababu ya kushuhudia kwa matendo makuu ambayo Mungu amemtendea katika maisha yake, Brenda alikuwa aanasumbuliwa na ugonjwa wa sickle cell kwa muda mrefu alipelekwa hospitalini na kutibiwa lakini ugonjwa huo haukumwacha na hali yake ilizidi kuwa mbaya. Ndipo ndugu yake alipoamua kumleta katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe iliyopo Tabata Segerea ili Yesu mtenda miujiza awatendee, walifika majira ya saa 9 alfajiri, alifika akiwa katika hali ya umauti kabisa maana alishakata tamaa kama anaweza kuishi tena.
Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph, akamwombea na kuifukuza roho ya kifo na sickle cell kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth ndani ya Brenda, naye akapokea uzima na kuwa huru mbali ya kuonewa na Ibilisi.
Hapa akiwa mzima baada ya kuombewa na Prophet Joseph kwa jina la Yesu Kristo.
Prophet Joseph akimpa maelekezo ya jinsi gani aendelee kutunza uponyaji wake.
Hapa akionekana mwenye nguvu maana hakuweza kutembea alikuja akiwa amebebwa lakini mara baada ya kupokea nguvu ya ufufuo anatembea mwenyewe.
Akishuhudia jinsi Mungu alivyomponya na kumtoa katika roho ya kifo.
Ndugu yake aliyemleta akimshukuru Mungu kwa aliyowatendea.
Brenda akitokwa na machozi ya furaha baada ya kurejeshewa uhai na Yesu Kristo wa Nazareth.
Hakika kuna nguvu ya ufufuo katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa Facebook ambao ni Life in Christ Ministries Zoe.
No comments:
Post a Comment