TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 2 November 2014

PINGILI ZA MGONGO ZAKAA SAWA KWA JINA LA YESU KRISTO

Mheshimiwa Ritha Mlaki mbunge viti maalum katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuja akiwa na tatizo la kupishana kwa pingili za mgongo kuanzia mwaka 2002 ambayo ilipelekea maumivu katika goti na mkono wake wa kulia na hakuwa anaweza kutembea sawasawa na ilibidi avae lumbar corset ili kupunguza maumivu. Alipokea uponyaji katika ibada ya Mass Deliverance iliyoongozwa na Prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu, mara baada ya maombi hayo alipokea uponyaji hapo hapo kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareth na kuwa mzima kabisa. UTUKUFU KWA YESU KRISTO.


                            Kabla ya maombi akiwa amevaa lumbar corset hiyo.


                             Mh. Ritha Mlaki akiwa mwenye furaha baada ya kupokea uponyaji.
                             Akiwa ni mwenye furaha tele baada ya maumivu kumwacha.
 Mh. Ritha Mlaki akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo pembeni ni msaidizi wake.
                                       Akitembea bila ya kuwa na maumivu yoyote.
               Akikunja mguu kuonyesha kuwa maumivu yamemwacha kwa Jina la Yesu Kristo.
                         Lumbar corset  ikiwa chini baada ya kupokea uponyaji .

                  Akimshukuru Mungu kwa kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.

                                SIFA NA UTUKUFU NI KWA YESU KRISTO.











No comments:

Post a Comment