Haijalishi mirija imeziba au madaktari wamesema nini juu yako kwa nguvu na uweza wa Mungu hakuna linaloshindikana. Ndivyo ambavyo ilikuwa kwa ndugu Esau Mbilinyi na mke wake, hakika walikuwa na kila sababu ya kumtukuza Mungu kwa jinsi alivyowatendea katika maisha yao.
Walikuwa wamekata tamaa mara baada ya kuhangaika kutafuta mtoto kwa zaidi ya miaka 5 bila ya kupata suluhisho, ndipo walipoamua kulileta tatizo hilo mbele ya Yesu Kristo mtenda miujiza. Walifika katika nyumba ya Mungu L.C.M Zoe kutokana na tatizo la kuziba mirija yote miwili ya uzazi ya Mrs. Esau Mbilinyi haikuwa rahisi kwa Mrs. Esau kuweza kubeba ujauzito kutokana na mirija hiyo kuziba.
Mwaka 2014 walifika na kupita kwenye mstari wa maombezi ( prayer line) mtumishi wa Mungu prophet Joseph aliwaombea na kuwauliza idadi ya watoto wanaotaka mara baada ya maombi walirudi nyumbani na kukutana kama mke na mume, hakika Mungu anajibu kama ukiamini waliamini na hakika Mungu aliwatendea.
Siku ya kujifungua ilipofika madaktari walipanga kumfanyia oparesheni lakini kwa neno la imani kutoka kwa mtumishi wa Mungu Prophet Joseph hawakuweza kumfanyia oparesheni na alijifungua kawaida pasipo kupasuliwa, mnamo saa 9 za alfajiri alijifungua mtoto wa kike mwenye afya tele. Kuwa na watoto ni ahadi ya Mungu kwetu sisi.
MR. NA MRS ESAU MBILINYI.
X-RAY IKIONYESHA MIRIJA ILIVYOKUWA IMEZIBA.
HUYU NDIYO MTOTO WA KIKE MWENYE AFYA TELE ALIYEZALIWA KWA MAOMBI.
VYETI VYA HOSPITALI KIKIONYESHA VIPIMO VYA MRS. ESAU.
Kumbukumbu la Torati 7:14 inasema ; Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mtu mume wala mke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa mifugo.
SIFA NA UTUKUFU KWA BWANA.
No comments:
Post a Comment