TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 21 September 2014

APOKEA UPONYAJI WA KIFUA NA SIKIO

Dada Catherine Mathew alikuja akiwa anasumbuliwa na matatizo ya kifua yaliyopelekea ashindwe kupumua vizuri na pia alikuwa na tatizo la kutokusikia vizuri kwa muda mrefu hakuweza kusikia kitu chochote kwa kutumia sikio hilo, lakini wakati mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alipoamuru kila minyororo ya ugonjwa iliyomshikilia mtu imwachie ndipo  dada Catherine aliweza kupokea uponyaji wake wa kifua na sikio hapo hapo.

                    Akieleza jinsi ambavyo alikuwa anasumbuliwa na magonjwa hayo.
Hapa tunaona akiwa ameziba sikio lake la kulia na Prophet Joseph akimwongelesha kwa mbali na yeye alisikia bila ya tatizo lolote,hii ni baada ya maombi.
Hapa akihema bila ya kuwa na matatizo ya kifua tena. Matatizo ya  kifua na sikio yakawa ni historia katika maisha yake.

Ahsante Yesu kwa kuendelea kuwaponya watu wako.

No comments:

Post a Comment