Hakika hakuna linaloshindikana kwa Mungu kaka yetu Claude alikuwa ameathirika na utumiaji wa madawa ya kulevya kwa muda wa miaka mingi na yeye kama yeye hakuweza kujitoa katika gereza hili kwa miaka yote hii, hali hii ilimtokea alipokuwa nchini Zambia kutokana na ushawishi wa marafiki akajikuta ameanza kutumia madawa ya kulevya aina ya Heroin. Aliporudi nchini Tanzania alishindwa kuacha kwahiyo ilimbidi aendelee kutumia. Kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho, ndipo alipoamua kuja katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe kwa ajili ya kufunguliwa na Yesu Kristo wa Nazareth akimtumia mtumishi wake Prophet Joseph.
Kutokana na utumiaji wa madawa ya kulevya hakuwa anaweza kupata usingizi ndipo Prophet Joseph alipoamuru aweze kupata usingizi kama tunavyoona kwenye picha hii akiwa amelala usingizi.
Akimshukuru Mungu kwa kumfungua kutoka katika kifungo cha utumiaji wa madawa ya kulevya.
SIFA NA UTUKUFU KWA MUNGU ALIYE JUU!!
No comments:
Post a Comment