TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Tuesday, 20 May 2014

MGUU ULIOVUNJIKA WAUNGA NA KUPONA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH.

Katika ibada ya jumapili 18/05/2014 ndugu huyu alikuja kwenye huduma ya Life in Christ Ministries Zoe,Tabata, Segerea Dar es salaam, akiwa katika hali ya maumivu makali yaliyotokana na ajali ya kugongwa na gari akiwa anaendesha pikipiki yake,ambapo ilipelekea kuvunjika mfupa wa mguu wa kulia na kuwekea chuma ambacho kwa ripoti ya madaktari ilimpasa kwanza kuwekewa chuma hicho kisha baada ya hapo kuwekewa hogo ili kuunganisha mfupa huo lakini ndugu huyu aliamua kuja katika huduma hii ili akutane na Yesu mponyaji asiyeshindwa kuunga mfupa wowote ule. Kwa kuwa jina la Yesu Kristo lina nguvu kupita majina yote alipofika katika huduma hii Prophet Joseph akiongozwa na roho alimtolea unabii kuwa ana roho ya ajali.Alifanyiwa maombi na mfupa ukaunga kabisa,alikuja anatembelea magongo mawili na mguu wake haukuweza kukanyaga chini lakini alipoombewa aliweza kukanyaga na pia kutembelea gongo moja kutokana na chuma alichokuwa amewekewa.Hakika Mungu anashangaza sana!


                                                                       Akiingia kanisani.

                    Akiwa amekaa kwenye kiti tayari kwa kuombewa na Prophet Joseph.
Prophet Joseph akimnyoshea mkono akiamuru maumivu kumwachia kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Prophet Joseph akiamuru roho chafu ya ajali iliyosababisha mguu kuvunjika imuache kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Prophet Joseph akiamuru mfupa uunge kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Prophet Joseph akiamuru nguvu ya ufufuo iliyomfufua Yesu Kristo katika wafu iingie kwenye eneo ambalo mfupa umevunjika na iunge mfupa na kuweka maeneo yote ya mifupa sawa.
Prophet Joseph akiamuru usaha uliochanganyika na damu ukauke kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Prophet Joseph akiamuru kisigino kilichopinda kikae sawa kwa jina laYesu Kristo wa Nazareth.
Prophet Joseph akiamuru goti lililokuwa limekaza ambalo lilikuwa likisababisha ashindwe kukanyaga chini na kushindwa kutembea liwe sawasawa na aweze kutembea kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Prophet Joseph akimwambia ndugu huyu kuwa amepona kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth na anaweza kutembea.
Prophet Joseph akimwambia ndugu huyu simama kwasababu maumivu yameshaondolewa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth na aanze kutembea.
Ndugu huyu akianza kutembea huku maelfu wakishuhudia muujiza huu mkubwa ambao Mungu ameutenda.
Prophet akimwambia ndugu huyu tembea Yesu Kristo amekuponya.
Ndugu huyu akimpa Yesu utukufu baada ya kuweza kutembea.

Ndugu huyu akishuhudia jinsi gani Yesu Kristo amemponya.

Maelfu wakimtukuza Mungu baada ya kumuona ndugu huyu anatembea.
Ndugu huyu akimshukuru Mungu jinsi gani ambavyo Mungu amemtendea huku gongo lake likiwa limeshikwa juu na mmoja kati ya mashemasi wa Life in Christ Ministries Zoe.

No comments:

Post a Comment