Mzee huyu alifika kwenye huduma ya Life in Christ Ministries Zoe, iliyopo jijini Dar es salaam, katika eneo la Tabata Segerea, akiwa ametoka mjini Moshi. Alifika akiwa na maumivu makali yaliyokuwa yakimsababisha ashindwe kukaa kwa taabu sana .Pindi alipofika kwenye huduma hii aliamini kuwa Mungu anatenda na atamtendea hata yeye. Ndipo Prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu alizungumza na mzee huyu na kisha kumnyoshea mkono na mzee kupokea uponyaji wake kupitia jina lililo kuu kupita majina yote,jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Akiingia kanisani.
Akisaidiwa na mwinjilisti wa huduma ya Life in Christ Ministries Zoe.
Akiwa amekaa akisikiliza neno la Imani.
Mzee huyu akielezea tatizo alilonalo.
Prophet Joseph akimnyoshea mkono akiamuru maumivu kumuacha mzee huyu kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Akiachia magongo baada ya maombi.
Akimtukuza Mungu kwa kumponya.
Mkewe naye akimshukuru Mungu kwa kumponya mumewe mpenzi.
Ndugu akibubujikwa na machozi ya furaha baada ya kuona ndugu yake akitembea bila ya msaada wa magongo.
Mzee akimshukuru Mungu kwa kumponya.