TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Tuesday, 13 May 2014

MUNGU ANAENDELEA KUTENDA HATA SASA......

Kijana huyu alikuja kwenye huduma ya Life in Christ Ministries Zoe akiwa anaamini kuwa Mungu atamponya mguu ambao ulikuwa umevunjika kutokana na kuanguka kutoka kwenye daladala aliyokuwa anafanyia kazi.Baada ya kuvunjika alienda katika hospitali ya Muhimbili ambapo alitakiwa kuwekewa chuma katika mguu wake ili mifupa iweze kuunga,lakini kutokana na kuamini kuwa Mungu wa Zoe anaendelea kutenda hata sasa aliamua moyoni mwake bila kushurutishwa na mtu kuwa lazima aje akutane na Mungu mtenda miujiza.Na alipofika tu katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe,Mungu alimtendea kama alivyoamini,wakati Prophet Joseph akiongoza maombi ya Mass Deliverance nguvu za Mungu zilimgusa na akaweza kulitoa hogo na kutembea bila ya msaada wa magongo.



                            Akibubujikwa na machozi ya furaha baada ya kupokea uponyaji.

                                              Akishuhudia jinsi Mungu alivyomtendea.


Baada ya kutoa hogo.

Akienda kuweka magongo na hogo katika ukuta wa uponyaji.


                                       Hogo likiwa limening'inizwa kwenye ukuta huo.
      Baadhi ya magongo,wheelchairs,neck colars,mahogo ambavyo watu walivitupa baada ya kupata      uponyaji.
                                       Akiwa amefika jumapili iliyofuatia akiwa ni mzima kabisa.
MKRISTO WA KWELI ANAJULIKANA KWA UPENDO WAKE.
Prophet Joseph akiongozwa na Yesu Kristo wa Nazareth aliweza kumkabidhi ndugu huyu shilingi laki mbili taslimu kutokana na hali ngumu aliyokuwa anapitia.
 
                                                Hapa akimshukuru Mungu.


No comments:

Post a Comment