Saturday, 28 June 2014
UGONJWA WA KANSA WASALIMU AMRI KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH.
Kaka huyu alikuja akiwa hawezi kutembea mwenyewe kutokana na ugonjwa wa kansa uliomsumbua kwa muda mrefu hadi kupelekea kukata tamaa kabisa,ilianza kama vidonda vya tumbo na alipokwenda hospitali walimweleza kuwa ni ugonjwa wa kansa, ndipo alipoona hakuna kimbilio lingine duniani isipokuwa kumkimbilia Yesu Kristo wa Nazareth yeye awezaye kuponya kila aina ya ugonjwa.
Saturday, 21 June 2014
ROHO YA UPOFU YAONDOLEWA KWA JINA LA YESU
Jumapili ya tarehe 15/06/2014 Prophet Joseph aliongoza maombi ya kuondoa roho ya upofu iliyokuwa ikiwanyemelea wana wa Mungu, mamia waliponywa macho waliokuwa hawaoni vizuri walipata kuona kwa jina la Yesu Kristo waliokuwa wanashindwa kusoma maneno madogo waliweza.
Baadhi ya watu waliofunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali ikiwamo kifungo cha upofu
katika ibada ya jumapili.
Baadhi ya watu waliofunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali ikiwamo kifungo cha upofu
katika ibada ya jumapili.
ZOE PARTNER OUTREACH
Katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe kuna vitengo mbalimbali kitengo kimojawapo ni kitengo cha Zoe partner ambacho kwa neema ya Mungu hushughulika na kutoa kwa watu mbalimbali wenye uhitaji au mahali penye uhitaji, kama tunavyoweza kuona kwenye picha hizi.Wakifanya matengenezo kwenye barabara mojawapo iliyopo katika eneo la Tabata Segerea iliyokuwa imeharibiwa na mafuriko.Reach out hii ilifanyika jumanne ya tarehe 17/06/2014.
Baadhi wa Zoe partners wakisambaza kifusi hicho.
Lori likimwaga kifusi tayari kwa matengenezo ya barabara.
Prophet akishindilia kifusi na mashine ya kushindilia.
Baadhi wa Zoe partners wakisambaza kifusi hicho.
Lori likimwaga kifusi tayari kwa matengenezo ya barabara.
Prophet akishindilia kifusi na mashine ya kushindilia.
Saturday, 14 June 2014
FIGO ZILIZOKUWA ZIMEKUFA ZAPONYWA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH
Hakuna ugonjwa ambao ni mkubwa kuliko jina la Yesu Kristo wa Nazareth, kwa kutaja jina hili lenye nguvu kupita majina yote kila ugonjwa unaondoka ndivyo ilivyokuwa kwa dada Beatrice aliyekuwa akisumbuliwa na figo kwa muda mrefu, ambapo figo zake zote mbili zilikuwa haziwezi kufanya kazi sawa sawa na kusababisha hadi kushindwa kujisaidia haja ndogo kwa urahisi. Alipelekwa hospitalini na kuwekewa dripu 36 lakini hakupata nafuu yoyote na pia hakuweza kula hata chakula kwa takribani wiki mbili, ndipo alipoamua kuja Life in Christ Ministries Zoe ili akutane na Yesu Kristo mtenda miujiza kwa kumtumia Prophet Joseph. Jumapili ya tarehe 1/8/2014 alifika akiwa hajiwezi kabisa kama ambavyo anaonekana kwenye picha.
Prophet Joseph akiamuru kila aina ya roho wa maumivu kumwachia dada Beatrice.
Nguvu ya Mungu ikifanya kazi ya kuondoa kila aina ya roho wa maumivu.
Dada Beatrice akimshukuru Mungu baada ya roho wa maumivu kumwacha kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Watu wakimshukuru Mungu kwa uponyaji wa dada Beatrice.
Baada ya kuondolewa roho wa maumivu ndipo ilipofuata awamu ya pili ya kuponywa figo zake zote na Yesu Kristo kupitia Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph.
Prophet Joseph akimwombea kwa kutumia jina la Yesu Kristo wa Nazareth ambaye kwake kila ugonjwa unatii.
Baada ya maombi Prophet Joseph akimwamuru kusimama maana alikuwa tayari ameshapokea uponyaji wake.
Dada Beatrice akimshukuru Mungu kwa kumpatia figo mpya .
Akilia kwa furaha na kumshukuru Mungu kwa kumrejeshea uhai katika figo zake.
Prophet Joseph akiwa na dada Beatrice.
Akitoa ushuhuda wa kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyomtendea katika maisha yake,hapa akiwa mwenye furaha na nguvu tele baada ya uponyaji, maana haikuwa rahisi kwake hata kusimama na kuongea kabla ya uponyaji lakini baada ya uponyaji anaonekana akiwa amesimama na kuongea akiwa na nguvu tele.
Maelfu ya watu waliokusanyika wakimtukuza Mungu kwa uponyaji huu.
Hatimaye baada ya kukaa wiki mbili bila ya kula baada ya maombi aliweza kusikia njaa na kuweza kula.
Hakika hakuna ugonjwa wowote ambao una nguvu kupita jina la Yesu Kristo, dada Beatrice alikuja akiwa hajiwezi kabisa lakini kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth kila kilichokuwa kimekufa ndani ya mwili wake kilifufuliwa na Yesu Kristo ambaye kwa jina lake kila aina ya mateso yanaondolewa. Mungu anaendelea kutenda hata sasa tunachotakiwa ni kuamini tu!!!