TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Thursday, 29 January 2015

MGUU ULIOTAKIWA KUKATWA NA MADAKTARI WAPONA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Jofari Barama kutoka Mombo la ndege jijini Dar es salaam, alikuja kwenye nyumba ya Mungu, Life in Christ Ministries Zoe akiwa na maumivu na akitembelea magongo kutokana na ajali ya pikipiki. Baada ya ajali hiyo ilipelekea mfupa katika mguu wake kuvunjika na kipande cha mfupa kupotea. Alipofika hospitalini madaktari baada ya kufanya vipimo wakamwambia ya kwamba hataweza kutembea tena katika maisha yake na inampasa mguu huo kukatwa. Lakini kwavile ripoti ya madaktari sio ripoti ya Mungu, kwa neema ya Mungu wakati mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akiamuru mifupa yote kuunga kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth alipokea uponyaji hapohapo. Ndipo alipopata nguvu za kutembea bila ya kutumia magongo. Maelfu waliofika katika nyumba ya Mungu LCM ,ZOE walibubujikwa na machozi ya furaha huku wakimshukuru Mungu kwa kumponya ndugu Jofari.


                                                 Ndugu Jofari Barama kwenye picha.
                                   Jofari Barama akiingia kwenye nyumba ya Mungu, LCM ZOE.
                    Mara baada ya kupokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.

                                              Akitembea bila ya msaada wa magongo.
                                                   Akibubujikwa na machozi ya furaha.
                                                   Akimtukuza Mungu kwa kumponya.
                           Mama huyu akitokwa na machozi ya furaha baada ya kuona muujiza huu.

 Wakitokwa machozi ya furaha kwa yale waliyoyaona jinsi Bwana Yesu Kristo alivyomtendea ndugu Jofari.
                                         Ndugu Jofari akimshukuru Mungu kwa kumponya.

Yesu Kristo wa Nazareth anaendelea kuponya hata sasa. Haijalishi madaktari wamesemaje kuhusu afya yako, Mungu akisema Ndio hakuna atakayesema Hapana. Mungu ndio msemaji wa mwisho. Jina la Bwana Libarikiwe.












Wednesday, 28 January 2015

WAFUNGULIWA KUTOKA KATIKA KIFUNGO CHA UNYWAJI WA POMBE...

Angel Otawa kutoka mkoani Kilimanjaro alikuwa kwenye kifungo cha unywaji wa pombe aina ya viroba kwa muda wa miaka 10 alijaribu kuacha kwa nguvu zake lakini ilishindikana, alipofika kwa Yesu Kristo ambaye kwake yeye hakuna linaloshindikana, kwa kumtumia mtumishi wake Prophet Joseph, Angel alifunguliwa na akawa huru kutoka katika kifungo hicho cha ulevi. Alifunguliwa katika mstari wa uponyaji mnamo tarehe 18/1/2015. 


                                     Angel akiwa kwenye mstari wa uponyaji ( Prayer line).

                           Akinywa kiroba hicho kuonyesha ni kweli huwa anatumia pombe hiyo.
                 Prophet Joseph akiifukuza kwa jina la Yesu Kristo, roho ya ulevi ndani ya dada Angel.



Mara baada ya maombi alishindwa kunywa pombe hiyo, hii ni kuonyesha kuwa yuko huru kutoka katika gereza hilo la ulevi.


2. Melvin Bihemo alifika katika ibada ya tarehe 18/1/2015 akiwa kwenye kifungo cha unywaji wa pombe aina ya Castle lager kwa miaka mingi, kwa neema ya Mungu alifunguliwa kutoka katika kifungo cha unywaji wa pombe.

                               Akinywa pombe hiyo kuonyesha kuwa hakika anatumia pombe hiyo.
                         Prophet Joseph akifukuza roho chafu ya pombe kwa ndugu Melvin.

                                                 Hakuna jambo gumu la kumshinda Bwana.






UPONYAJI WA PAPO HAPO...

Verynice Elisante kutoka kijitonyama, jijini Dar es salaam alifika siku ya Jumatano katika darasa la Imani linalofundishwa kila siku ya jumatano na mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph, akiwa na maumivu makali yaliyotokana na mfupa wa mkono wa kushoto uliokuwa umevunjika. Madaktari walimshauri kuwa ni lazima awekewe chuma katika mkono huo ili mfupa uunge. Verynice hakuona kama itakuwa sawa kwake kuwekewa chuma kutokana na ndoto yake ya kuwa mwanajeshi pindi atakapomaliza masomo yake, ndipo alipoweka tumaini lake kwa Yesu Kristo na kuamini kuwa pindi atakapofika hapa LCM ZOE mfupa utaunga bila ya kuwekewa chuma. Hakika Yesu Kristo kwa kumtumia mtumishi wake Prophet Joseph kumponya, mkono wa dada Verynice uliunga papo hapo.

                                     Verynice Elisante akielezea kuhusiana na mkono wake.
                     Prophet Joseph akiamuru mfupa kuunga kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
                  Mara baada ya maombi akiondoa kifaa kilichokuwa kikimsaidia kushikia mkono huo.
Verynice akiwa ametoa kifaa kilichokuwa kinamsaidia kushikilia mkono huo, huku mtumishi wa Mungu prophet Joseph akiushika mkono huo.


                                    Akiwa mwenye furaha mara baada ya kupokea uponyaji.
                                          Akilia machozi ya furaha kwa kupokea uponyaji.

Rafiki yake Verynice akishangaa baada ya kuona matendo makuu ya Mungu aliyomtendea rafiki yake, kabla ya uponyaji huu rafiki huyu hakuwa akiamini kuwa Yesu Kristo yu hai na anaweza kuponya, lakini mara baada ya kuona muujiza huu aliamini kuwa hakika Yesu Kristo yu hai na anatenda hata sasa.



Monday, 26 January 2015

SHUHUDA WAKATI WA KIPINDI CHA MASS DELIVERANCE

Asma Barabara alikuja katika ibada ya jumapili 25/1/2015 akiwa hawezi kutembea sawasawa, kutokana na tukio lililomtokea mwezi mmoja uliopita. Mwezi mmoja uliopita majira ya saa 6 za usiku akiwa anamfungulia mchumba wake mlango mara alipatwa na hali ya kizunguzungu na kuanguka chini, alipoanguka chini hakuweza kusimama wala kutembea ndipo mdogo wake na kaka yake wakamwinua na kumpeleka hospitalini, alipewa dawa lakini maumivu yalibaki palepale. Wakati wa kipindi cha kufunguliwa kwa pamoja (Mass deliverance) wakati mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph akifukuza kila aina ya roho chafu kwa jina la Yesu Kristo dada Asma alipokea uponyaji na kutembea bila ya kuwa na maumivu ya aina yoyote.

                                     Akishuhudia matendo makuu ya Mungu aliyomtendea.
                                        Akimshukuru Bwana Yesu Kristo kwa kumponya.
                                Akikimbia bila ya kuwa na maumivu mara baada ya uponyaji.
                            Akiwa ni mwenye furaha huku akimtukuza Mungu kwa kumtendea.

                          MUNGU TUNAYEMTUMIKIA ANATENDA HATA SASA UKIAMINI.


MAUMIVU YA NYONGA YA MIAKA 11 YAONDOKA KWA JINA LA YESU KRISTO

Jacqueline Minja amepokea uponyaji wa nyonga kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth, amekuwa na maumivu ya nyonga na miguu kwa miaka 11 alitumia dawa lakini hazikumsaidia, kwa neema ya Mungu aliweza kupokea uponyaji na kuwa huru kabisa kutoka katika kifungo cha roho chafu ya maumivu.

   Dada Jacqueline akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
                                        Akitembea bila ya kuwa na maumivu yoyote yale.
 Dada Jacqueline,mtoto wake na Prophet of God,Prophet Joseph wakimshukuru Mungu kwa uponyaji.

Wakibubujikwa machozi ya furaha baada ya Yesu Kristo kumtoa katika mateso ya muda mrefu.

Hakuna jambo lolote gumu ambalo Yesu Kristo hawezi kufanya... Yeye ni Yule Jana, Leo na Hata Milele.

                                       UTUKUFU NI KWA YESU KRISTO.








Monday, 19 January 2015

APOKEA UPONYAJI MARA TU BAADA YA KUSIKIA NENO LA UZIMA.

Katika Biblia Takatifu, kitabu cha Warumi 10:17 inasema " Imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo".

Katika ibada ya jumapili 18/1/2015 mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alikuwa akifundisha juu ya maisha ya Mungu ndani yetu (ZOE) na kusema kuwa pindi mtu anapopata neema ya kuwa na maisha ya Mungu ndani yake magonjwa yanakuwa si sehemu yake. Ndugu Francis Mwaluwanda aliyekuwa amepata ajali, baada ya pikipiki aliyopanda kugongwa na daladala uso kwa uso na kusababisha mfupa wa mguu wake kuvunjika na alipokwenda hospitali ya Sinza na Mwananyamala kote ilishindikana na akahamishiwa katika hospitali ya Muhimbili, pindi alipolisikia neno la uzima lililokuwa likifundishwa na mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph juu ya maisha ya Mungu ndani yetu, ndugu Francis uzima uliingia katika mguu wake palepale na kupokea uponyaji wa mguu maana alikuja akiwa anatembelea magongo lakini mara baada ya kulisikia neno la uzima lenye uvuvio wa Roho Mtakatifu aliweza kusimama bila ya kutumia magongo.
 Kwa kuthibisha kama ni kweli mfupa wake ulikuwa umevunjika kwa utukufu wa Mungu, Afisa wa afya kutoka wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam alikuja kusoma X ray ya ndugu Francis na kuthibitisha ni kweli ndugu Francis mfupa wake ulikuwa umevunjika. Na ndugu Francis alitakiwa kufanyiwa upasuaji  tarehe 19/1/2015 katika hospitali ya Muhimbili kitengo cha mifupa MOI ili kumwekea vyuma kama antenna.
Lakini kwa uaminifu wa Mungu alipokea uponyaji na kutupa magongo na akatembea bila ya msaada wa magongo kwavile magongo si sehemu ya maisha yake.



                                 Ndugu Francis akishuhudia matendo makuu ya Mungu.
                  Ndugu zake na ndugu Francis wakishuhudia matendo makuu ya Mungu.
                                                       X -ray ya ndugu Francis.
                             Ndugu Francis akikimbia bila ya kuwa na maumivu ya aina yoyote.

 Ndugu wakitokwa na machozi ya furaha baada ya kuona jinsi ambavyo Bwana Yesu Kristo amemponya ndugu yao.
                                  Magongo yakitundikwa juu kwa ajii ya ushuhuda.

                         Magongo si sehemu ya ndugu Francis yanabaki kuwa ushuhuda tu.

                                           JINA LA BWANA LIBARIKIWE.

FANGASI ZA MUDA MREFU ZAKOMA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Kwa miaka 11 dada Dorice Georvine ameteseka na fangasi za sehemu za siri lakini kwa neema ya Mungu alifika katika nyumba ya Mungu Life in Christ Ministries Zoe,ili aweze kupokea uponyaji kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Fangasi hizi ziliharibu mfumo wake wa mayai,alipokwenda hospitalini alipewa dawa lakini hazikumsaidia,pia fangasi hizi zilisababisha hata asiweze kupata ujauzito, pia kutokana na fangasi hizo alimbidi kuvaa nguo za ndani mbili,pedi au vitambaa kutokana na kutokwa na maji sehemu zake za udada maji yenye harufu kali. Mara baada ya kufunguliwa Prophet Joseph aitoa neno la kinabii kwa Dorice ya kwamba kuanzia sasa maji yaliyokuwa yakimtoka sehenu zake za udada hayatamtoka tena na aende chooni akajikague hakika alipokwenda kujikagua akakuta hakuna maji yoyote yaliyokuwa yanamtoka, maji yenye harufu yalikoma palepale kwa jina la Yesu Kristo mtenda miujiza.

                                                 Pichani ni dada Dorice.
                                               Akielezea kuhusu fangasi hizo.
 Prophet Joseph akiamuru kila roho chafu ya fangasi kumwacha dada huyu kw ajina la Yesu Kristo wa Nazareth.
 Akimshukuru Yesu Kristo kwa kumweka huru, huku akielekea chooni kujikagua.

Hiki ni kitambaa ambacho alikuwa akikiweka sehemu ya udada ili kuzuia maji yaliyokuwa yakimtoka lakini kwa utukufu wa Mungu, alipokwenda kujikagua akakuta maji yale hayatoki tena kama alivyokuwa ametoa neno la kinabii mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph.

Hakuna ugonjwa ambao Yesu Kristo hawezi kuuponya. Libarikiwe jina la Yesu Kristo.







AFUNGULIWA KUTOKA KATIKA KIFUNGO CHA KUNYWA MAFUTA YA TAA NA KUTAFUNA HELA...

Nguvu za Mungu za kuwatoa watu kutoka katika vifungo vya aina mbalimbali zinaendelea kuonekana hata sasa. Hakika tunakila sababu ya kumtukuza Mungu.
Agness Richard alikuwa kwenye kifungo cha kunywa mafuta ya taa na kutafuna hela za noti kwa miaka 7. Mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema kuwa anachikiona kwa dada huyu ni zaidi ya kunywa mafuta ya taa,na kwamba pia dada Agness alikuwa na tatizo katika ubongo wake amayo humletea hali ya kuchanganyikiwa, ndipo mtumishi wa Mungu prophet Joseph akielekezwa na RohoMtakatifu alisema dada huyu atafunguliwa mara mbili kwanza ni kutoka katika kifungo cha kunywa mafuta ya taa na kutafuna hela na kufunguliwa kwa mara ya pili ni kutoka katika hali ya kuchanganyikiwa.


                                                   Mafuta ya taa aliyokuja nayo.

                                  Dada Agnes akiwa ameshikiliwa chupa ya mafuta ya taa.

Mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu akaendelea kusema kuwa hali hii inampata dada huyu akiwa kwenye siku zake ndipo dada Agnes alipokiri kuwa ni kweli hali hii humtokea akiwa katika siku zake.
    Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akimfungua dada Agness kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.

Pia mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alisema mpango aliokuwa nao adui kwa dada Agness ni kumpa kansa ya tumbo lakini mara baada ya maombi,prophet Joseph alitoa neno la kinabii ya kwamba dada Agness hatakaa apate kansa ya tumbo kamwe kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.


                Hapa Prophet Joseph akitumia jina la Yesu Kristo kumweka huru kutoka katika hali ya kuchanganyikiwa.

Dada Agness akimshukuru Yesu Kristo wa Nazareth kwa kumweka huru kutoka katika vifungo vyote vya adui.

Mwanzo 18:14- inasema; Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Hakika hakuna neno gumu la kumshinda Bwana tumeendelea kuona nguvu za Mungu zikiwatoa watu kutoka katika vifungo vya aina zote, Hakika Yesu Kristo ni Bwana wa Mabwana.

                                           Utukufu kwa Yesu Kristo wa Nazareth.