TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 14 February 2015

AFUNGULIWA KUTOKA KATIKA KIFUNGO CHA KULA UDONGO,KUVUTA SIGARA NA UNYWAJI POMBE

Lydia John alikuwa kwenye kifungo kilichomtesa kwa muda mrefu kifungo cha kula udongo, kuvuta sigara na unywaji wa pombe alikuwa akivuta sigara pakiti moja kwa siku, baada ya kushindwa kuacha kwa nguvu zake mwenyewe ndipo alipoamua kuja kwa Yesu Kristo maana kwake hakuna linaloshindikana, alikuja katika mstari wa uponyaji (Prayer Line) jumapili ya tarehe 1/2/2015 na Yesu Kristo hakumuacha arudi kama alivyokuja, alifunguliwa kabisa na kuwa huru kutoka katika maonevu yote ya ibilisi. Utukufu kwa Mungu juu.

                               Lydia John akiwa kwenye mstari wa uponyaji ( Prayer Line).
                          
                                                Akieleza jinsi ambavyo hula udongo huu.
                                       Huu ndio udongo aliokuwa akitumia dada Lydia.
                     Mtumishi wa Mungu, akiondoa kila roho chafu ndani ya dada Lydia.


 Jumapili ya tarehe 8/2/2015 alifika katika huduma ya LCM ZOE kushuhudia jinsi Mungu alivyobadili maisha yake.

                                                     Lydia John baada ya kufunguliwa.
Akiwa ni mwenye furaha tele baada ya kufunguliwa na Yesu Kristo wa Nazareth na kupata maisha mapya.

No comments:

Post a Comment