TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Monday, 20 April 2015

TUMBO LILILOVIMBA LANYWEA KWA JINA LA YESU KRISTO

Leonard Steven alifika akiwa na tatizo la kuvimba tumbo na hii ilikuwa ikimpa maumivu makali ya tumbo. Tatizo hili lilianza miezi mitatu iliyopita mwanzo iliona kama ni halli ya kawaida lakini hali ilipozidi kuwa mbaya akaamua kutafuta msaada wa matibabi lakini haikusaidia. Kutokana na tatizo hili hakuweza kula kwa siku kadhaa na akila alikuwa akila chakula kidogo sana na hakuwa akipata haja kwa siku 3 hadi 5. Lakini kwa nguvu za Mungu alipokea uponyaji na maumivu yote yalimwacha na tumbo lilianza kunywea.

                               Ndugu Leonard akiingia kwenye nyumba ya Mungu LCM Zoe.
                                              Hivi ndivyo tumbo linavyoonekana.
                                               Akiwa ndani ya nyumba ya Mungu.
                                     Akishuhudia jinsi maumivu ya tumbo yalivyomwacha.



Sunday, 12 April 2015

MWANAMKE ALIYEKUWA AKITOKWA NA DAMU KWA MIAKA 22 APOKEA UPONYAJI WAKE KUTOKA KWA YESU KRISTO WA NAZARETH



Zuhura Nyalusi alikuwa na kila sababu kuja kumshukuru Mungu kwa yale aliyomtendea katika maisha yake na familia yake. Zuhura alikuwa na tatizo la kutokwa na damu kwa muda wa miaka 22 bila kukoma maana hii ilikuwa ni zaidi ya mwanamke wa kwenye biblia aliyekuwa akitokwa na damu kwa muda wa miaka 12 Luka 8:43  hadi 48. Alikwenda sehemu nyingi kutafuta jawabu ya tatizo lake lakini bila ya msaada na ndio kwanza tatizo lilizidi, tatizo hili lilimuanza pale alipoota akifanya mapenzi na marehemu baba yake mzazi  na alipoamka alijikuta akiwa amechafuka kana kwamba alikuwa amezini na mwanaume.
Alikwenda hopsitalini walichukua vipimo lakini hawakuona tatizo lolote lakini damu ilendelea kutoka. Ndipo mtumishi wa Mungu prophet Joseph akatupa fundisho ya kwamba hakuna mawasiliano ya aina yoyote kati ya walio hai na waliolala mauti na pili kila mtu anapoota ndoto za aina hiyo ni lazima ukatae na kuvunja kwa jina la Yesu Kristo. Mama Zuhura alindelea kuelezea kwamba kutokana na tatizo hilo hakuwa na hamu yoyote na marehemu mume wake na ilipelekea walale katika vyumba tofauti maana aliendelea kuota ndoto za kufanya mapenzi na watu tofauti tofauti. Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alimwombea kwa jina la Yesu Kristo na damu ilikoma palepale na fahamu ya viungo vyake vya mwili ikarudi.
Alifika katika darasa la imani siku ya jumatano na kupokea uponyaji wa miguu alikuwa na uzito katika miguu yake lakini Yesu Kristo alimfungua, pia mtoto wake alipata neema ya kufunguliwa kutoka katika roho ya hasira.
                                             Zuhura akishuhudia jinsi Mungu alivyomponya.
Zuhura akiwa na binti yake aliyesimama upande wa kushoto ambaye naye alifunguliwa kutoka katika roho ya hasira.

                                   HAKUNA JAMBO GUMU LA KUMSHINDA MUNGU.


Thursday, 9 April 2015

DAMU ILIYOKUWA IKIMTOKA KWA MUDA WA MIEZI MIWILI YAKOMA KWA NGUVU YA UFUFUO

Rolesta Kilunda kutokea Temeke, alikuja akiwa na tatizo lakutokwa na damu kwa miezi miwili mfululizo bila kukoma, ingawa anafanya kazi ya uuguzi lakini hakuweza kujitibu mwenyewe alitumia kila aina ya dawa lakini damu haikukoma, alikuwa akitumia pedi na vitambaa  lakini damu iliendelea kutoka kwa wingi ilikuwa ikimtoka hadi kuchafua nguo zake. Alifika katika nyumba ya Mungu LCM Zoe kwa nguvu ya ufufuo  iliyomfufua bwana wetu Yesu Kristo kutoka mauti iliweza kusimamisha mateso yote kwa dada Rolesta. Afisa muuguzi wa huduma alikwenda naye chooni kumkagua na kweli akahakikisha kuwa hakika damu imekoma na kuwa dada Rolesta amepokea uponyaji.

 Kushoto ni watenda kazi katika nyumba ya Mungu katikati ni dada Rolesta kulia ni afisa muuguzi wa huduma.

               Afisa muuguzi akishuhudia kwamba ni kweli damu imekoma kwa dada Rolesta.

                   Akionyesha pedi ikiwa ni ishara ya kwamba ni kweli damu haimtoki tena.
                                               Akimshukuru Mungu kwa kumponya.




Tuesday, 7 April 2015

KWA NENO LA KINABII AJIFUNGUA BILA YA OPARESHENI WALA KUONGEZEWA DAMU

Upendo Petro alifika kwenye mstari wa uponyaji wiki moja kabla ya kwenda kujifungua, alipokuwa kwenye mstari wa uponyaji aliweza kupata ujumbe kutoka kwa Mungu kwa kupitia mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph ya kwamba dada Upendo alikuwa na tatizo la kuishiwa damu  na kwamba haijalishi atajifungua salama na bila ya kupasuliwa. Na ndivyo ilivyokuwa alifika katika nyumba ya Mungu LCM Zoe kushuhudia matendo makuu ya Mungu na kushuhudia kilichotokea. Alipofika hopsitalini madaktari walimweleza kuwa itakuwa ngumu kujifungua kutokana na upungufu wa damu alionao kwa wakati huo damu ilikuwa 9 na baada ya muda iliteremka na kufikia damu 6 wakati madaktari wakijiandaa kwa ajili ya upasuaji aliomba ruhusa ili aweze kupiga simu katika nyumba ya Mungu LCM Zoe, alipiga na walimpa neno la imani ya kwamba aendelee kuamini kwamba atajifungua salama na bila kupasuliwa kama alivyonena mtumishi wa Mungu, prophet Joseph. Aliendelea kukiri neno la imani wakati madaktari wakiendelea kujiandaa aliomba ruhusa ili aende chooni lakini walimkatalia na wakamweleza kuwa ajisaidie hapohapo kitandani, naye alitii lakini haikuwa kama madaktari walivyosema hakika neno la Mungu ni kweli na hakika akiwa kitandani alijifungua palepale bila ya kupasuliwa wala kuongezewa damu na bila ya maumivu yoyote. Alifika mbele ya nyumba ya Mungu akiwa ni mwenye afya yeye pamoja na mtoto wake, alifika kushuhudia ukuu wa Mungu katika maisha yake. Na pia alifika kumuuliza mtumishi wa Mungu juu ya jina gani ampe mtoto wake huyo, mtumishi wa Mungu alimwambia amwite God yaani amani ya Mungu.


                                         Dada Upendo akiwa na mtoto wake.
                     Prophet Joseph akiwa amempakata mtoto God.
                                           Mtoto God akiwa ni mwenye afya tele.

               Mtumishi wa Mungu prophet Joseph akimkabidhi dada Upendo mtoto God.

                                          HAKUNA LA KUMSHINDA BWANA.








Monday, 6 April 2015

KIFAFA CHA MIMBA NA PRESHA YA JUU VYAONDOLEWA KWA JINA LA YESU KRISTO

Mungu wetu anatenda hata sasa, Brenda Mushi alifika katika nyumba ya Mungu LCM Zoe kumshukuru Mungu kwa kumponya, alifika akiwa na matatizo ya presha ya juu na kifafa cha mimba, presha ilikuwa ikipanda inafika hadi 160/100 alikwenda hospitalini ambapo madaktari walimshauri kuwa anywe maji mengi ili presha yake irudi chini lakini haikusaidia kitu tatizo lilibaki palepale. Alirudi tena hospitalini ambapo walimpa uhamisho wa kwenda kwenye hospitali ya Temeke ili apate matibabu zaidi, alifika na aliandikiwa dawa, kila siku alitakiwa kumeza vidonge 54 lakini moyoni mwake alikuwa akiomba kwamba Mungu ambaye Prophet Joseph anamtumikia asimwache katika tatizo hilo, alifika katika maombi na hakika Mungu hakumwacha alipokea uponyaji wake. Alipokwenda hospitalini presha ilikuwa imeshuka kabisa na kufikia 120/70 na ugonjwa wa kifafa cha mimba ukawa umemuacha kabisa.

                                                           Dada Brenda Mushi 
                                      Dada Brenda akiwa na afisa muuguzi wa huduma.

                               Cheti kabla ya maombezi kikionyesha presha ikiwa juu 160/100.
     Cheti cha hospitali kikionyesha presha ikiwa imekuwa kawaida 120/70 hii ni baada ya maombezi.




KESI NA KIFUNGO CHA NJE VYOTE VYAFUTWA KWA JINA LA YESU KRISTO

Wilson Sigalla alikuwa na kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kile alichomtendea katika maisha yake, ndugu Wilson alikuwa akiishi Afrika ya kusini na alikuwa na kesi iliyopelekea kufungwa gerezani mara baada ya kutumikia kifungo hicho kwa muda aliachiliwa na kuanza kutumikia kifungo cha nje ambacho alitakiwa kukitumikia kwa miaka miwili, kwa neema ya Mungu aliweza kufika kwenye huduma ya Life in Christ Ministries Zoe na alipita kwenye mstari wa uponyaji hakika Mungu hakumwacha kwa kuwekea mkono tu na mtumishi wa Mungu Prophet Joseph kila uonevu wa ibilisi katika maisha yake ulikoma. Mara baada ya maombi kesi ilifutwa na yuko huru kabisa.


                                             Ndugu Wilson akimtukuza Mungu kwa kumwokoa.

                                                   UTUKUFU KWA BWANA WETU YESU KRISTO.


Saturday, 4 April 2015

KIFUNGO CHA ULEVI CHAMWACHA KWA JINA LA YESU KRISTO

Peter Mayunga aliwekwa huru kutoka kwenye kifungo cha unywaji wa pombe, amekuwa kwenye kifungo hiki kwa muda mrefu, alijaribu kuacha kwa akili zake lakini haikuwa rahisi kwasababu roho chafu ya ulevi ilikuwa nyuma ya tatizo hilo. Hakuna awezaye kujitoa kwenye kifungo chochote bila ya msaada wa Yesu Kristo.

                                   Akiwa kwenye mstari wa uponyaji (prayer line).
           Prophet Joseph akifukuza roho chafu ya ulevi ndani ya ndugu Peter Mayunga.
                               Mara baada ya maombi akijaribu kuinywa pombe hiyo.
                        Hakuweza kuinywa kabisa hii ni kuonyesha kuwa yuko huru kabisa.
Akiitupa pombe hiyo kwenye pipa la takataka hakika Yesu Kristo akikuweka huru unakuwa huru kweli kweli.

APOKEA UPONYAJI WA HIV NA MGUU KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

 Kila ugonjwa ni lazima usalimu amri kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth, na haijalishi ni tatizo gumu kiasi gani ambalo unapitia, Yesu Kristo ndio jibu pekee kama ukiamini nguvu zilizomo kwenye jina hili kuu lipitalo majina yote.

Ndugu Patric Peter kutoka Mlandizi yeye ni mjenzi wa majumba alipata ajali ya kuanguka kutoka juu ya nyumba aliyokuwa akijenga na kusababisha mguu wake kuteguka. Ni kwa neema tu aliweza kusikia matangazo ya huduma ya LCM Zoe yanayorushwa kwenye Radio Uhuru Tz na akaamua moyoni mwake kuwa ni lazima afike ili akutane na Yesu Kristo mtenda miujiza. Alifika na hakika kama ambavyo aliamini moyoni mwake kuwa atapokea uponyaji na ndivyo ilivyokuwa, aliweza kupokea uponyaji wa mguu na uponyaji wa HIV aliyokuwa nayo.

               Akiwa sehemu ya mapokezi tayari kwa kuingia kwenye nyumba ya Mungu.

                            Mara baada ya kupokea uponyaji akienda mbele kushuhudia.
 Akishuhudia jinsi ambavyo amepokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.
                 Ndugu Patric aliweza kukunja mguu mara baada ya kupokea uponyaji wake.
                             Pia aliweza kuchuchumaa bila ya kuwa na maumivu yoyote.

                                                      UTUKUFU KWA YESU KRISTO.


ATUPA MAGONGO MARA BAADA YA KUPOKEA UPONYAJI WA NYONGA KUTOKA KWA YESU KRISTO

Asha Issa kutoka Ukonga, Banana alikuja na maumivu makali ya nyonga amekuwa kwenye mateso hayo kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na alikuwa akitembelea magongo kutokana na maumivu hayo lakini alipofika katika nyumba ya Mungu Life in Christ Ministries Zoe alipata uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.

                                              Akitembea bila ya msaada wa magongo.
                                         Magongo yakiwa juu kwa utukufu wa Mungu.
            Akitupa magongo chini hii ni kuonyesha ishara ya kuwa amepokea uponyaji wake.
Haya ndio magongo aliyokuwa akitumia dada Asha kabla ya kupokea uponyaji sasa yakiwa chini hii ni kuonyesha kuwa hakika Bwana Yesu Kristo amekwisha muweka huru na haihitaji tena magongo.

                                             UTUKUFU KWA YESU KRISTO.




Thursday, 2 April 2015

MATESO YA MIAKA 2O YAMWACHA KWA JINA LA YESU KRISTO

Ellylumba Mshana alikuja akiwa anatembelea kifaa maalum cha kutembelea kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo, presha pamoja na maumivu makali kwenye magoti yake kwa zaidi ya miaka 20, amekwenda kwenye hospitali nyingi lakini tatizo lilikuwa palepale. Alifika katika nyumba ya Mungu LCM akiamini kabisa kuwa sasa ni wakati wa Mungu kumponya na ndivyo ilivyokuwa, Mungu hakumwacha alimponya na kuwa huru kabisa.

                                            Akishuka kwenye usafiri uliomleta.
                              Akiingia kwenye nyumba ya Mungu. LCM Zoe.
                                         Akitembea kwa kutumia kifaa maalum.

                                      Akilia kwa furaha mara baada ya kupokea  uponyaji.
                                      Akitembea bila ya msaada wa kifaa cha kutembelea.

                                                  Mungu wetu ni Mungu atendaye hata sasa.

MKONO ULIOVUNJIKA WAUNGA

 Kila jumapili Mungu anaendelea kumtumia mtumishi wake, Prophet Joseph kwa ishara, maajabu na miujiza. Jumapili hii tuliweza kushuhudia miujiza mingi ya kushangaza kutoka kwa Yesu Kristo kupitia Prophet Joseph. Ndugu Hashim Jumanne alipata ajali ya pikipiki na kusababisha mfupa katika mkono wake kuvunjika, alipokwenda hospitali madaktari walimwekea chuma na hogo ili mfupa wake uweze kuunga, Kwa neema ya Mungu alisikiliza neno lililokuwa likifundishwa na prophet  Joseph neno lenye uvuvio wa Roho Mtakatifu na kwa kuamini tu mkono uliunga papo hapo.


                                                          Ndugu Hashim pichani.
                 Akiwa akiingia katika nyumba ya Mungu tayari kupokea uponyaji wake.
                                 Ndugu. Hashi akiwa kwenye nyumba ya Mungu.
                                            Akishuhudia jinsi alivyopokea uponyaji.
                     Akinyosha juu mkono kuonyesha kuwa maumivu yameshamwacha.
Aliweza kukunja mkono mara baada ya kupokea uponyaji.

Hiki ni kifaa alichokuwa amekiweka mkononi ili kushikizia hogo mara baada ya maombi alikitupa kuonyesha kuwa hakika amekwisha kuwa mzima.

 P.O.P likiondolewa katika mkono wake mara baada ya uponyaji . Halihitaji tena maana si sehemu ya maisha yake.

                                                                Baada ya kutoa P.O.P .