Zuhura Nyalusi alikuwa na kila sababu kuja kumshukuru Mungu kwa yale aliyomtendea katika maisha yake na familia yake. Zuhura alikuwa na tatizo la kutokwa na damu kwa muda wa miaka 22 bila kukoma maana hii ilikuwa ni zaidi ya mwanamke wa kwenye biblia aliyekuwa akitokwa na damu kwa muda wa miaka 12 Luka 8:43 hadi 48. Alikwenda sehemu nyingi kutafuta jawabu ya tatizo lake lakini bila ya msaada na ndio kwanza tatizo lilizidi, tatizo hili lilimuanza pale alipoota akifanya mapenzi na marehemu baba yake mzazi na alipoamka alijikuta akiwa amechafuka kana kwamba alikuwa amezini na mwanaume.
Alikwenda hopsitalini walichukua vipimo lakini hawakuona tatizo lolote lakini damu ilendelea kutoka. Ndipo mtumishi wa Mungu prophet Joseph akatupa fundisho ya kwamba hakuna mawasiliano ya aina yoyote kati ya walio hai na waliolala mauti na pili kila mtu anapoota ndoto za aina hiyo ni lazima ukatae na kuvunja kwa jina la Yesu Kristo. Mama Zuhura alindelea kuelezea kwamba kutokana na tatizo hilo hakuwa na hamu yoyote na marehemu mume wake na ilipelekea walale katika vyumba tofauti maana aliendelea kuota ndoto za kufanya mapenzi na watu tofauti tofauti. Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alimwombea kwa jina la Yesu Kristo na damu ilikoma palepale na fahamu ya viungo vyake vya mwili ikarudi.
Alifika katika darasa la imani siku ya jumatano na kupokea uponyaji wa miguu alikuwa na uzito katika miguu yake lakini Yesu Kristo alimfungua, pia mtoto wake alipata neema ya kufunguliwa kutoka katika roho ya hasira.
Zuhura akishuhudia jinsi Mungu alivyomponya.
Zuhura akiwa na binti yake aliyesimama upande wa kushoto ambaye naye alifunguliwa kutoka katika roho ya hasira.
HAKUNA JAMBO GUMU LA KUMSHINDA MUNGU.
No comments:
Post a Comment