TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 10 May 2015

KISUKARI SUGU CHAOONDOLEWA KWA NGUVU YA MUNGU

Esther Makweta ana kila sababu ya kumshukur Mungu kwa yale ambayo Mungu amemtendea katika maisha yake. Alifika katika nyumba ya Mungu Lcm Zoe April 5 mwaka 2015 akiwa na kidonda kikubwa katika mguu wake kutokana na kusumbuliwa na kisukari kwa muda mrefu. Sukari ilikuwa inapanda hadi kufikia 24-26, kutokana na kisukari kidonda katika mguu wake hakikuweza kupona haraka . Alipewa rufaa ya kwenda katika hospitali ya taifa Muhimbili ili wakaukate mguu huo kwavile haikuwezekana kupona, mara zote madaktari hufikia hatua ya kukata mguu ili kuokoa sehemu ya ubongo isiathirike kutokana na donda hilo. Lakini wakati mtumishi wa Mungu prophet Joseph akiongoza maombi ya pamoja ndugu Esther alipokea uponyaji wake papo hapo, alikwenda hospitali madaktari walishangaa sana mara baada ya vipimo maana kiwango cha sukari kilikuwa 8.


                                      Akiwa kwenye nyumba ya Mungu LCM Zoe, tarehe 5/4/2015.


                                                          Kidonda hicho kilivyokuwa.
                       Afisa muuguzi wa huduma akielezea kwa upana juu ya mguu huu. Hii ni jumapili   ya tarehe 10/5/2015 mara baada ya maombi.

                              Hivi ndivyo ambavyo mguu unaonekana mara baada ya maombi.

Katika picha ni vyeti vya hospitalini vinavyoonyesha vipimo ambavyo ndugu Esther alivifanya.

                                                       SIFA NA UTUKUFU KWA YESU KRISTO.



No comments:

Post a Comment