TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 22 March 2014

HAKIKA MUNGU ANAENDELEA KUZUNGUMZA NA MANABII WAKE HADI SASA...

Prophet of God,Prophet Joseph alitoa unabii kuhusiana na dada mmoja ambaye alivamiwa na roho ya kutaka kumuua baba yake...


Ndipo dada huyu alipotoka na kukiri ni kweli yote ambayo Nabii wa Bwana amenena yako sahihi kabisa.

                                 Baba mzazi akithibitisha unabii alioutoa Prophet Joseph.

                                       Dada huyu akiwa ameshikilia kisu hicho....
                                         WAKATI  WA KUWEKWA KWAKE HURU...


                         
Akifurahia baada ya kuwekwa huru na Yesu Kristo.
         

                      BABA MZAZI NAYE AKIWEKWA HURU KWA JINA LA YESU KRISTO.



                                                       Prophet Joseph akimuombea...

   

                      Prophet Joseph akiendelea kumfungua kwa kutumia Jina la Yesu Kristo.

                                                    Baba na Mama wa Anna
                                                  Wakimchezea Mungu baada ya kufunguliwa.

Thursday, 20 March 2014

ZOE REACH OUT(ZOE LOVE PARTNERSHIP)


Hivi ni baadhi ya vyakula ambavyo ni kwa neema ya Mungu huduma ya life in Christ Ministries iliweza kutoa kwa watu mbalimbali wenye uhitaji kama neno la Mungu linavyosema katika maandiko matakatifu .Matendo ya mitume 20:35
Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge,na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu,jinsi alivyosema mwenyewe,Ni heri kutoa kuliko kupokea.


Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia,kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji,akamzuilia huruma zake,je!Upendo wa Mugu wakaaje ndani yake huyo? Waraka wa kwanza wa Yohana 3:17




Mmoja kati ya wainjilisti wa life in Christ Ministries Zoe,Mwinjilisti Joyce akifurahia kutoa,kama Prophet Joseph ambavyo husema wakati wa kutoa ni wakati wa kufurahia
1 Wakorintho 13:13,Basi, sasa inadumu imani,tumaini,upendo haya matatu;na katika hayolililo kuu ni upendo.

Prophet of God prophet Joseph akijazililizia mchele kwenye viroba tayari kwa kwenda kugawiwa.
Kwa maana mlikuwa na njaa mkanipa chakula;nalikuwa na kiu,mkaninywesha;nalikuwa mgeni,mkanikaribisha.Mathayo 25:35.
                                       Prophet Joseph akitoa kwa kufurahi....
Mmoja kati ya wainjilisti wa huduma ya L.C.M ZOE.

Saturday, 8 March 2014

MSTARI WA MAOMBI (PRAYER LINE)







UNABII

Amos 3:7 Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lolote,pasipo kuwafunulia watumishi manabii siri yake.
Kila jumapili, Mungu anazungumza na watu kupitia Prophet Joseph.Mungu anaweka wazi siri za adui na mipango ya Mungu kwenye maisha ya watu.vilevile,Mungu anazungumza juu ya kusudio la Mungu katika maisha ya watu.Roho wa Mungu anamtumia Prophet Joseph kuzungumza juu ya mipango yanchi na hata dunia nzima.
Mfano tumemsikia Mungu akitoa unabii juu ya MV spice,mafuriko ya Morogoro,ajali za ndege mbalimbali.

MAFUNDISHO

Yohana 4:24, Mungu ni roho,nao wamwabudio yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Zoe tunafundisha imani sio dini (Waebrania 11:6 Basi pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu) Imani inasisitiza upendo,msamaha,uvumilivu,na unyenyekevu.Inakupa ujasiri wa kujua kwamba unaye Mungu mwenye nguvu anayeweza kuwashindia lolote na kuwapa lolote,hapo tutakapo amini (yote yawezekana kwake yeye aaminiye) Roho wa Mungu huwa anamuongoza Prophet Joseph kufundisha kweli ya Mungu na jinsi watu wanavyoweza kulitumia neno hili kuwa washindi siku zote dhidi ya magonjwa,umaskini,uonevu wa adui (Waefeso 6:12 kwa maana hatupambani na binadamu,bali tunapambana na tawala na mamlaka na nguvu za ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.) Karibu ujifunze neno sahihi la Mungu na uwe mshindi siku zote.    

Thursday, 6 March 2014

KUFUNGULIWA

Yohana 14:10, Husadiki ya kwamba mimi ndani ya Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwashauri langu; lakini baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.Watu wengi wanaaingia katika huzuni,Chuki,upweke,umaskini,magonjwa na wamejikuta hawana msaada.Mungu yupo na shetani naye yupo.Mpango wa mungu katika maisha ya kila mtu ni kuwa na afya njema,amani,furaha,upendo,kufanikiwa na kustawi katika kila jambo.Mpango wa adui ni kuchinja,kuua,na kuharibu kila jambo jema ambalo mtu anafanya.Lakini shetani anatambua kwamba hana nguvu mbele ya Mungu na anajisalimisha kwa jina la yesu kristo (Marko 1:21-28) kila jumapili watu wanawekwa huru na vifungo mbalimbali chini ya jina lenye nguvu na mamlaka la yesu kristo.Yesu kupitia mtumishi wake,Prophet Joseph anawafungua watu na vifungo mbalimbali kama kula udongo,mchele,ndoto za kufanya mapenzi,kukabwa usiku,umaskini,kuchanganyikiwa,na usagaji.

Je wewe ni jambo gani unataka Mungu akufungue limekuwa kero kwako.Kumbuka hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu. Karibu ili Yesu abadilishe maisha yako moja kwa moja.











UPONYAJI

Yohana 14:12 Amin,Amini, nawaambieni, yeye aniaminiaye mimi kazi nizifanyazo mimi,yeye naye atazifanya;naam kubwa kuliko hizo atafanya..."
Yesu Kristo ndiye mponyaji.LCM  tunashuhudia Yesu akiwaponya watu magonjwa mbalimbali ambayo yameshindikana kama Kansa,Ukimwi,Presha,Kisukari,mifupa kuvunjika n.k. Hakuna ugonjwa ambao Mungu hawezi kuponya,kwa sababu yote yawezekana kwake.Watu wanaponywa kupitia mstari wa uponyaji "Prayer Line" na ibada nzima ya jumapili kutegemea jinsi ambavyo roho wa Mungu anavyomwongoza Mtumishi wake.Wengi wamekuja kushuhudia jinsi ambavyo Mungu amebadilisha maisha yao moja kwa moja.

              Mama huyu akitoa maelezo ya tatizo lake kabla ya kuombewa na Prophet Joseph

                                                      Baada ya Maombezi
      

       Ndugu huyu akiingia kwenye ibada katika kanisa la Life in Christ Ministries Zoe,aliyekuwa amepata ajali ya pikipiki na aliamini kuwa Mungu ataenda kumponya.


Akiombewa na mtumishi wa Mungu Prophet Joseph


                                    USHUHUDA-Baada ya maombezi hakika Mungu anatenda hata sasa.

                                   

HISTORIA YA ZOE







Zoe life in Christ Ministries ( LCM) ni huduma ya kinabii,Makao Makuu yake yakiwa  Tabata/Segerea,Dar es salaam Tanzania.Huduma hii ilianza baada ya mtumishi wa Mungu Prophet Joseph,kuitwa na Mungu kuongoza huduma ya watu zaidi ya 70,000.Huduma ilianza miaka minne na watu watano tu.Sasa hivi inapokea zaidi ya watu 1000 kwa wiki.
LCM hatufundishi dini bali imani.tunapokea watu kutoka dini mbalimbali kama vile, Wakatoliki,Walutheri,Waislamu,Wahindi,Wayahudi na hata Wapagani wasiomjua Mungu.Tunaamini ya kwamba watu wote hawa wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na hatuna mamlaka ya kuwahukumu au kuwatenga na upendo wa Mungu ambao unafundishwa katika kanisa lake.Tunaamini kanisa ni sehemu ya kupokea kila mtu jinsi alivyo,kwani Mungu anampenda kila mtu kama alivyo.

Yeremia 29:11 maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi,asema BWANA,ni mawazo ya amani wala si ya mabaya,kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho

Ukiona wewe ni mtu mwenye dhambi karibu sana kanisani kwetu.Yesu Kristo hakuja kwa waliosafi,bali wenye dhambi ili awaokoe.(Luka 5:32),Sikuja kuwaita wenye haki,bali wenye dhambi,wapate kutubu.