TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 8 March 2014

MAFUNDISHO

Yohana 4:24, Mungu ni roho,nao wamwabudio yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Zoe tunafundisha imani sio dini (Waebrania 11:6 Basi pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu) Imani inasisitiza upendo,msamaha,uvumilivu,na unyenyekevu.Inakupa ujasiri wa kujua kwamba unaye Mungu mwenye nguvu anayeweza kuwashindia lolote na kuwapa lolote,hapo tutakapo amini (yote yawezekana kwake yeye aaminiye) Roho wa Mungu huwa anamuongoza Prophet Joseph kufundisha kweli ya Mungu na jinsi watu wanavyoweza kulitumia neno hili kuwa washindi siku zote dhidi ya magonjwa,umaskini,uonevu wa adui (Waefeso 6:12 kwa maana hatupambani na binadamu,bali tunapambana na tawala na mamlaka na nguvu za ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.) Karibu ujifunze neno sahihi la Mungu na uwe mshindi siku zote.    

No comments:

Post a Comment