TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 29 November 2014

MAELFU WALIOFUNGULIWA KUTOKA KATIKA VIFUNGO MBALIMBALI

Hawa ni baadhi tu  ya maelfu waliofunguliwa kutoka katika vifungo vya kula mchele,makaratasi,barafu,mkaa,chaki,mifuko ya plastiki na vitu vingi vichafu lakini kwa upendo wa Mungu wetu waliwekwa huru na Yesu Kristo na hapa wakishuhudia toka wamefunguliwa hawana hamu ya kula tena vitu hivyo vichafu.



Baadhi tu ya waliofunguliwa kutoka katika kifungocha kula vitu vichafu. Sifa kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

KWA HABARI ZAIDI TEMBELEA UKURASA WETU WA FACEBOOK LIFE IN CHRIST MINISTRIES ZOE. AHSANTENI.

SHUHUDA


Maelfu walishuhudia na kumshukuru Mungu jinsi ambavyo amewatoa katika vifungo vya ulevi na uvutaji sigara wa muda mrefu.


                                    Yanayoshindikana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana.

AFUNGULIWA KUTOKA KATIKA KIFUNGO CHA MUME WA KIPEPO (SPIRITUAL HUSBAND)

Mungu ni mwenye upendo na rehema sana kwetu dada Neema Mbajo alikuwa katika mateso ya muda mrefu kuanzia akiwa katika kidato cha tatu alikuwa akiota anafanya mapenzi na mwanaume asiyemfahamu, ikafikia hatua akawa akimuona mwanaume huyo kinadharia, yaani mwanaume huyo alikuwa akimtokea bila ya kuota. Siku moja akiwa anatembea njiani ndege wawili walikuja na kutua kichwani kwake na kuanza kupigana mara akaanguka na kuzimia alikwenda sehemu nyingi lakini hakupata msaada. Alipomaliza shule aliolewa lakini kutokana na kuwa na mume wa kipepo ndoa yake iliharibika. Pia alijaribu kufungua biashara mbalimbali lakini hazikufanikiwa kutokana na mume huyu wa kipepo kumuharibia biashara na maisha yake. Alipofika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe, Yesu Kristo mtenda miujiza alimfungua kwa kupitia mtumishi wake Prophet Joseph na kuwa huru  kabisa kutoka katika mateso ya muda mrefu.

                                              Akielezea jinsi roho hiyo chafu ilivyomtesa.

Hakuna jambo gumu la kumshinda Yesu, yeye ni Alfa na Omega ( ni mwanzo tena mwisho)                                                             Utukufu kwa Yesu Kristo.

USHUHUDA WA MASS DELIVERANCE

Leticia Musore kutoka Tabata alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mbavu,kifua,kiuno na miguu, Alifika kushuhudia jinsi Yesu Kristo wa Nazareth alivyomponya, wakati wa mass deliverance mtumishi wa Mungu Prophet Joseph aliamuru kukataa magonjwa mama huyu pindi alipokataa magonjwa aliwekwa huru na Yesu Kristo na maumivu yote yakamwacha kwa jina la Yesu Kristo.

Akishuhudia jinsi ambavyo Yesu Kristo amemponya na kumfungua kutoka katika kifungo cha roho ya maumivu. Ahsante Yesu Kristo.






MKONO WAUNGA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Mama huyu alifika akiwa amefungwa POP mkononi, sababu iliyopelekea kufungwa na POP ni kwamba akiwa nyumbani kwake alisikia kizunguzungu  na kuanguka chini alipoanguka alivunja vidole vyake vya mkononi. Lakini kwa Neema ya Mungu alipofika katika ibada ya jumapili 23/11/2014 alipokea uponyaji wake mara moja kutoka kwa Yesu Kristo.



                             Mama huyu akiingia katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe.


                              Akinyoosha mkono juu bila ya kuwa na maumivu yoyote yale.
            Afisa wa afya kutoka katika Hospital ya wilaya Temeke akikagua mkono wa mama huyu na kuthibitisha kuwa ni kweli mama yetu amepokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo.
                           Mama huyu akimshukuru Mungu kwa kumponya mkono wake....

                                                  HAKIKA YESU ANAWEZA.

NGUVU YA UPONYAJI KATIKA JINA LA YESU KRISTO

Kuna nguvu ya uponyaji katika jina la Yesu Kristo, haijalishi tatizo linalokusumbua ukiamini kuwa Yesu Kristo anaweza kukuponya hakika atakuponya. Mama huyu alikuja akiwa na maumivu katika mguu wake uliopelekea kupata kidonda kikubwa katika mguu huo lakini aliamini kuwa hakika Yesu Kristo atamponya wakati wa maombi ya Mass deliverance mtumishi wa Mungu Prophet Joseph aliamuru roho za maumivu na magonjwa kuwaacha watu kwa jina la Yesu Kristo ndipo mama huyu akapokea uponyaji wake.


                                                           Mguu huo unavyoonekana.

MAGONGO YATUPWA KWA JINA LA YESU KRISTO

Atupele kutoka Mafinga, Iringa alikuwa na maumivu makali katika mguu wake na kusababisha ashindwe kutembea pasipo msaada wa magongo. Madaktari walimweleza kuwa mfupa wake wa mguu umepishana. Lakini wakati wa Mass deliverance iliyoongozwa na Prophet Joseph mama huyu aliweza kutembea bila ya msaada wa magongo. Hakika Mungu ni mwema sana.


                                   Mama huyu  akitembea bila ya msaada wa fimbo.
                                              Akishuhudia matendo makuu ya Mungu.

Gongo hilo likiwa limeshikwa juu na mmoja wa watenda kazi katika huduma hii ya Life in Christ Ministries Zoe, ikionyesha kuwa mama huyu ni mzima na haihitaji kutembelea gongo tena. UTUKUFU KWA BWANA WETU YESU KRISTO.

Saturday, 22 November 2014

NENO LA KINABII KATIKA MAISHA YA WATU

Maelfu wanaofika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe hupata neema ya kusikia neno la kinabii linalotoka kwa Mungu mwenyewe akimtumia mtumishi wake Prophet Joseph, Prophet anapotoa neno la kinabii si neno lake bali ni neno kutoka kwa Mungu mwenyewe kama biblia inavyosema katika kitabu cha   
2 Petro 1:20-21 inasema; 20. Awali ya yote,yawapasa mjue kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama apendavyo mtu mwenyewe. (21.)Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya wanadamu ,bali watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Neno la kinabii huleta amani,furaha,suluhisho kufunguliwa na kuwekwa huru.

Kaka yetu alipata neema ya kusikia kutoka kwa Mungu kupitia Prophet Joseph. Kaka yetu alikuwa kila anachofanya hakifanikiwi na amekuwa akiota mtu anamfukuza na pia Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akiongozwa na Roho aliendelea kumweleza kuwa amekuwa akiota anapanda treni lakini tofauti na ilivyozoeleka amekuwa akiota anapanda treni ya mbele kaka huyu ndipo alipokiri kuwa ni kweli mambo yote hayo ndiyo yanayomtokea kwenye maisha yake.
Ikafika wakati wa kaka huyu kuwekwa huru na Yesu Kristo wa Nazareth.



                                   Akiwekwa huru kutoka katika mateso hayo yote.

2. Mama huyu naye alipata neema hiyo ya kusikia kutoka kwa Mungu kupitia Prophet Joseph, Prophet alimwendea mama huyu na kumweleza kuwa amekuwa akisubuliwa na kifua kuuma na mbavu kubana kwa muda mrefu na hadi kupelekea mama huyu kudhania kuwa anasumbuliwa na Asthma mama huyu akakiri ni kweli kabisa, lakini Prophet Joseph akiongozwa na Roho aliendelea kumweleza mama huyu kuwa si ugonjwa wa Asthma kama mama huyu anavyodhani bali ni uonevu wa shetani, na pia alimweleza mama huyu kuwa anasumbuliwa na presha ya chini mama huyu alimshangaa Mungu sana na kusema ni kweli kabisa anapitia mambo yote hayo.
                                    Akifunguliwa kutoka katika roho chafu za magonjwa.

3. Mama huyu pia alipata neno la kinabii kuwa amekuwa akipatwa na hasira za mara kwa mara jambo dogo tu humfanya apandwe hasira kwa haraka mama huyu akakiri ni kweli kabisa na amejaribu kuacha ameshindwa kabisa ndipo ulipofika wakati wa Yesu Kristo kumweka huru kabisa kutoka katika roho chafu ya hasira.


                           Akikiri kuwa ni kweli amekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu.

              Prophet Joseph akimfungua kwa jina la Yesu Kristo kutoka katika hali hiyo.

4. Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alimwendea kaka yetu na kumweleza kuwa kaka huyu amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya magoti kwa muda mrefu amekuwa akishindwa kuinama au kuchuchumaa kaka yetu akakiri ni kweli kabisa amekuwa akipata maumivu hayo.



              Prophet Joseph akiifukuza roho ya maumivu kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
                                      Roho hiyo ya maumivu ikimwacha kaka huyu .

5. Pia mama huyu alipata neema ya kusikia kutoka kwa Mungu, Prophet Joseph alimfwata mama huyu na kumwambia kuwa mama huyu amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo na mabega mara kwa mara mama huyu alikiri kuwa ni sahihi kabisa anayosema mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph.

MAMA HUYU AKIWEKWA HURU KUTOKA KATIKA ROHO HIYO CHAFU YA MAUMIVU

                                Akiwa amechukuliwa na nguvu ya Mungu.
                           Prophet Joseph akimfungua mama huyu.

Mungu anaendelea kuzungumza na watu wake kupitia watumishi wake. Utukufu na Sifa ni kwake yeye mwenye uwezo na nguvu zote! Jina la Bwana Libarikiwe!!!

Tuesday, 18 November 2014

SHUHUDA ZA TOTAL DELIVERANCE

Total Deliverance ni kufunguliwa kwa watu kutoka katika vifungo vya kula vitu ambavyo kwa hali ya kawaida watu wengi hufikiri kuwa ni kawaida au ni ukosefu wa madini fulani mwilini ambao ndio unapelekea watu kula vitu hivyo kama makaratasi,mkaa,udongo,vifuniko,barafu,pencil,chaki,peni,mchele n.k lakini huu ni uonevu wa ibilisi kuwafanya watu kula vitu hivi kinyume na Mungu alivyowaumba, pia ni kufunguliwa kutoka katika utumiaji wa pombe za aina zote uvutaji wa sigara,bangi, na utumiaji madawa ya kulevya ya aina zote na kufunguliwa kutoka katika hali ya ushoga,usagaji ,upigaji punyeto (masturbation). Na hakika tumemuona katika huduma hii ya Life in Christ Ministries Zoe Mungu akiwatoa watu kutoka katika vifungo hivi vyote kupitia mtumishi wake Prophet Joseph. Yesu pekee ndiye mwenye uweza na nguvu ya kuwafungua watu kutoka katika vifungo hivi.
Hizi ni baadhi tu ya shuhuda za watu waliofunguliwa katika ibada ya Jumapili 16/11/2014.


         Ndugu waliokuja kufunguliwa na Yesu Kristo kutoka katika mateso ya aina mbalimbali.

Ndugu Halubu Omary alikuwa katika kifungo cha utumiaji wa madawa ya kulevya kwa takriban miaka 10, alikuwa hawezi kulala bila ya kutumia madawa hayo na afya yake ilikuwa ikizorota kila siku kutokana na utumiaji wa madawa hayo. Kwa Neema na Upendo wa Mungu aliweza kufika katika ibada ya Jumapili na kuingia katika  Total deliverance na kufunguliwa moja kwa moja kutoka katika roho ya utumiaji wa madawa ya kulevya.

                    Ndugu Halubu akielezea jinsi ambavyo anateseka na utumiaji wa madawa.

Mtumishi wa Mungu, Prophet Joseph akifukuza roho chafu ya madawa ya kulevya kumwacha ndugu Halubu.

                            Roho chafu ikimwacha ndugu Halubu kwa jina la Yesu Kristo.
                     Roho hiyo chafu ya utumiaji wa madawa ya kulevya ikiwa imemwacha ndugu Halubu.
          Akiwa huru kutoka katika kifungo hicho....Sifa na Utukufu ni kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

2. Dada Theofrida alikuwa katika kifungo cha kupiga punyeto (Masturbation),kula udongo na unywaji wa pombe aina ya Konyagi viroba kwa  muda mrefu lakini Mungu ni mwema sana aliweza kufunguliwa na Yesu Kristo kutoka katika vifungo hivyo.

                      Dada Theofrida akionyesha udongo huo na jinsi ambavyo alikuwa akila.
                  Hapa akinywa kiroba kuonyesha kuwa ni kweli alikuwa akinywa pombe hiyo.
 Mtumishi wa Mungu,Prophet Joseph akifukuza roho hizo chafu kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth kumwacha dada huyu.

                   BAADA YA KUFUNGULIWA KUTOKA KATIKA VIFUNGO HIVYO.
 Mara tu baada ya kufunguliwa kutoka katika utumiaji wa pombe hakuweza tena hata kuionja pombe hiyo.
                                                  Pia hakuweza kuula udongo huo tena.

3.  Dada Avelina alikuwa kwenye kifungo cha kula mchele kwa muda mrefu alijaribu kwa uwezo wake wote kuacha kula mchele lakini alishindwa kuacha kwa nguvu zake, ndipo alipoamua kufika Life in Christ Ministries Zoe ili afunguliwe na Yesu Kristo wa Nazareth akimtumia mtumishi wake Prophet Joseph.

                                     Akielezea jinsi ambavyo hali hiyo humtokea.
                                     Akiwa ameshikilia mchele huo.
                                Hapa akionyesha jinsi ambavyo huutafuna mchele huo.
                Mtumishi wa Mungu,Prophet Joseph akifukuza oho hiyo chafu kwa jina la Yesu Kristo.
                                   Baada ya kufunguliwa akitapika mchele huo.

                            Baada ya kufunguliwa hakuweza kuula mchele huo tena .

Hakuna nguvu inayoweza kumtoa mtu kutoka katika vifungo hivi isipokuwa ni nguvu ya jina la Yesu Kristo. Hivyo tunakila sababu ya kumshukuru na kumtukuza Mungu wetu.

Saturday, 15 November 2014

HAKIKA MUNGU HASHINDWI NA JAMBO


Asu Ntetemela alikula chakula na alipomaliza alipata allergy, mwili wake wote ulivimba na kuanza kuwasha. Ndipo alipoamua kumweleza mama yake juu ya hali iliyomkuta na kisha wakaamua kumpigia simu Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph, Mtumishi wa Mungu akwamwambia atumie maji kufuta mwili wake na baada ya dakika tano uvimbe wote utakwisha, akatumia maji na baada ya muda mfupi uvimbe ule ukapungua kwa kiasi kikubwa.

Lakini baada ya muda akaamua kutumia barafu kukanda sehemu ya uvimbe uliobakia, hii ikiwa ni kunyume na maagizo kutoka kwa Prophet Joseph, uvimbe ule ukazidi na kuwa katika hali mbaya pindi alipotambua kosa lake kuwa alikuwa akimsahihisha Mungu alitubu haraka. Maana Prophet anapozungumza,anazungumza kwa niaba ya Mungu si maneno yake mwenyewe.
Siku iliyofuata alipata maelekezo kutoka kwa Prophet Joseph kuwa atumie Annointing Oil kwenye mikono yake na miguu alipotumia uvimbe na muwasho wote ukaisha pale pale kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
 

   
                                          Hivi ndivyo kaka yetu Asu alivyokuwa.
                          Hapa ni baada ya uponyaji akishuhudia jinsi Mungu alivyomponya.

                            Bwana wetu Yesu Kristo hashindwi na jambo lolote. Halleluya!!!!