Donny George amefika kwenye nyumba ya Mungu Life in Christ Ministries Zoe,kumshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyomtendea katika maisha yake, mke wake alikuwa mjazito kwa wiki 12 lakini hakuwa na uchungu muda wa kujifungua ulipofika. Walipofika hospitalini madaktari walimshauri kwamba lazima mke wake afanyiwe oparesheni ili aweze kujifungua. Kwa neema ya Mungu ndugu Donny akatumia mafuta ya upako (Annointing Oil) aliyopewa na prophet Joseph, baada ya muda mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akamwelekeza mkewe Donny aweke mkono kwenye tumbo lake baada ya maelekezo kutoka kwa prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu mkewe Donny akapata neema ya kujifungua kwa salama bila ya kufanyiwa oparesheni ya aina yoyote jambo ambalo limewashangaza sana madaktari na kuacha historia katika hospitali ya Aga Khan kwasababu haijawahi kutokea mtu kujifungulia kwenye ward na sio chumba maalum cha kujifungulia, alijifungua bila ya maumivu yoyote hakika Mungu ni mwema sana katika maisha yetu.
Ndugu Donny akishuhudia na kumshukuru Mungu.
No comments:
Post a Comment