TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 28 June 2015

ZOE!!! OUR SERVICE HAS JUST STARTED HERE AT LIFE IN CHRIST MINISTRIES HEAD QUARTERS AT TABATA SEGEREA. WE ARE ALSO BROADCASTED LIVE ON UHURU FM. RADIO 95.7 FM DAR ES SALAAM OR www.uhurufm,co,tz. JUST TUNE THERE AND BE BLESSED AS YOU LISTEN LIVE SERVICE.

Saturday, 20 June 2015

MAUMIVU YA NYONGA YA MUDA MREFU YASALIMU AMRI KWA JINA LA YESU KRISTO

Elisa Kamugisha alikuwa na maumivu ya nyonga ya kulia kwa muda wa miaka 23 na kumsababishia maumivu makali na kutembelea magongo, alikwenda kwenye hospitali mbalimbali ndani na mwisho akapewa rufaa ya kwenda kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi, alifanyiwa uchunguzi mara 5 na ndipo madaktari walipomweleza kuwa kuna viashiria vya kansa katika mwili wake kama hiyo haikutosha akaamua kwenda kwenye hospitali ya wamarekani iliyopo nchini Tanzania na kuamua kwenda kufanya vipimo. Walimfanyia vipimo na kubaini kuwa ana tatizo katika figo zake wakamwandikia dawa na akawa akitumia dawa hizo lakini hazikusaidia.Alipojaribu kila aliloweza kwa uwezo wake na kushindwa ndipo alipoamua kumtafuta Daktari wa madaktari, Yesu Kristo wa Nazareth. Alipofika katika nyumba ya Mungu LCM Zoe alikutana na mtenda miujiza Yesu Kristo kwa kumtumia mtumishi wake Prophet Joseph , na hakika Mungu hakumwacha alimponya na akapokea uzima papo hapo.


                        Akiingia kwenye nyumba ya Mungu tayari kupokea uponyaji wake.
                                       Anavyoonekana katika picha akiwa na magongo.
                                                        Akitembea bila ya magongo.
                                       Magongo yakiwa juu na akitembea mwenyewe.
                                      Akishuhudia matendo makuu ya Mungu.

Kupokea uponyaji kutoka kwa Mungu ni sekunde tu endapo utaamini manabii wake na kazi ambazo Yesu Kristo anatenda hata sasa kupitia wapakwa mafuta wake. Hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu wala hakuna ugonjwa ambao hawezi kuuponya kwake yeye kuna spea zote. Kwa imani tu utafunguliwa kutoka katika kila aina ya kifungo.

                                                 UTUKUFU KWA MUNGU JUU!!!

Monday, 8 June 2015

MIFUPA YAUNGA KWA JINA LA YESU KRISTO MPONYAJI

Felista Ludela alikuwa akivuka barabara katika eneo la Tazara jijini Dar es salaam, lakini wakati akivuka pikipiki ilimgonga na kusababisha mfupa wa mkono wake kuvunjika. Alikwenda hospitali wakamfunga kifaa maalum ili mfupa uweze kuunga. Kwa neema ya Mungu dada Felista aliweza kufika katika nyumba ya Mungu Life in Christ Ministries Zoe, wakati wa kipindi cha kuabudu  Yesu Kristo mtenda miujiza alimponya na kuweza kuondoka kifaa hicho katika mkono wake na maumivu yote yalimwacha palepale. 

                                                 Jinsi alivyoingia kwenye nyumba ya Mungu.
                                             Akionekana ni mwenye maumivu hii ni kabla ya maombi.

                       Akiondoa kifaa hicho katika mkono wake wakati wa kipindi cha kuabudu.
                          Akiwa ameondoa kifaa hicho mara baada ya kupokea uponyaji.
                                            Akimshukuru Mungu kwa kumponya.
                                               Akishuhudia jinsi Mungu alivyomponya.
Kifaa hicho kikiwa chini kuonyesha kuwa hakihitaji tena katika maisha yake, na ni ishara kuwa Mungu amemponya kabisa.

                                                           UTUKUFU KWA MUNGU!!!

Thursday, 4 June 2015

MIFUPA YAUNGA HATA SASA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Reginald Peter alipata ajali ya gari na kuvunja mfupa wa mguu wake wa kushoto (Fibula na Tibia) alifanyiwa upasuaji na kuwekea chuma ili kuwezesha mifupa kuunga lakini mfupa huo haukuweza kuunga na kusababisha maumivu makali katika mguu wake. Pia hakuwa akiweza kukanyaga chini kwa kutumia mguu huo, alikuja akiwa anatembelea magongo mawili. Alifika katika mstari wa uponyaji na mtumishi wa Mungu prophet Joseph kwa uweza na nguvu za Mungu alimwekea mkono ndugu Reginald naye akapokea uzima kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kuanza kutembea bila ya msaada wa magongo.



 Akishuka kwenye usafiri uliomleta na akipokelewa na mmoja wa watenda kazi wa Lcm Zoe.
                                       Anavyoonekana na magongo kwenye picha.
                                            Mguu ukiwa na pop unavyoonekana.
                                                       Akiwa na magongo.
                                             Akiwa kwenye mstari wa uponyaji.
                                     Prophet Joseph akimwekea mkono ndugu Reginald.

                                             Akisimama bila ya msaada wa magongo.
                      Prophet Joseph akikemea roho ya maumivu kumwacha ndugu Reginald.
                            Akikanyaga chini kwa mara ya kwanza baada ya maombezi.
Akitembea na magongo yakiwa juu hii ikionyesha kuwa hakika Yesu Kristo amemponya kabisa.

                                        UTUKUFU KWA MUNGU MWENYE UWEZA.

Tuesday, 2 June 2015

UVIMBE WA MGUU WANYWEA KWA JINA LA YESU KRISTO

Anitha Machume alifika katika nyumba ya Mungu LCM Zoe akiwa amevimba mguu wake wa upande wa kulia. Alikuwa amepumzisha mwili alipoamka alikuta mguu wake umevimba , wakati wa ibada ya kufunguliwa kwa pamoja ( Mass deliverance) nguvu ya Mungu ilimchukua na kujikuta yuko chini. Mtumishi wa Mungu prophet Joseph alifika na kuamuru uvimbe na kila roho chafu kumwacha kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth na pale pale uzima uliingi ndani ya ndugu Anitha na akasimama na kutembea kawaida wakati mwanzo alikuwa akitembea kwa shida sana na pale pale uvimbe ukaanza kunywea. Kaka yake alipoona jinsi Mungu alivyomponya dada yake alishangaa matendo makuu ya Mungu na alimshukuru Mungu sana.

                              Mguu huo ulivyokuwa ukionekana kabla ya maombezi.
                            Ndugu Anitha akiwa ndani ya nyumba ya Mungu.
                      Akiwa chini mara baada ya kuchukuliwa na nguvu ya Mungu.
                       Prophet Joseph akimwombea kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
                        Akiwa chini na mguu ukiwa unonekana jinsi ulivyovimba.
                              Mara baada ya maombezi akitembea bila ya maumivu.
                                                 Akielezea alivyopokea uponyaji.
                         Kaka yake Anitha akimshukuru Mungu kwa kumponya dada yake.

                                             SIFA NA UTUKUFU WA MUNGU.

HAKUNA LINALOSHINDIKANA KWA BWANA

Godson Barnabas alifika katika nyumba ya Mungu, Life in Christ Ministries zoe akiwa na tatizo la ugonjwa wa moyo, mishipa ya moyo ilikuwa imepanuka na kusababisha kutokuweza kutembea bila ya msaada wa chuma cha kutembelea. Alipita kwenye mstari wa uponyaji na mtumishi wa Mungu prophet Joseph akamwekea mkono na nguvu ya ufufuo ikamponya ndugu Godson na kuwa huru kabisa.

                                  Ndugu Godson akiwa na fimbo kabla ya maombezi.
                                                Akiwa kwenye mstari wa uponyaji.
                        Prophet Joseph akifukuza roho ya udhaifu ndani ya ndugu Godson.
                                         Akisimama mara baada ya maombezi.
                                                  Akitembea bila ya msaada wa fimbo.

Ndugu Godson akiwa huru kabisa kutoka katika kila kifungo, hakuna linaloshindikana kwa Yesu Kristo wa Nazareth.