TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 20 June 2015

MAUMIVU YA NYONGA YA MUDA MREFU YASALIMU AMRI KWA JINA LA YESU KRISTO

Elisa Kamugisha alikuwa na maumivu ya nyonga ya kulia kwa muda wa miaka 23 na kumsababishia maumivu makali na kutembelea magongo, alikwenda kwenye hospitali mbalimbali ndani na mwisho akapewa rufaa ya kwenda kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi, alifanyiwa uchunguzi mara 5 na ndipo madaktari walipomweleza kuwa kuna viashiria vya kansa katika mwili wake kama hiyo haikutosha akaamua kwenda kwenye hospitali ya wamarekani iliyopo nchini Tanzania na kuamua kwenda kufanya vipimo. Walimfanyia vipimo na kubaini kuwa ana tatizo katika figo zake wakamwandikia dawa na akawa akitumia dawa hizo lakini hazikusaidia.Alipojaribu kila aliloweza kwa uwezo wake na kushindwa ndipo alipoamua kumtafuta Daktari wa madaktari, Yesu Kristo wa Nazareth. Alipofika katika nyumba ya Mungu LCM Zoe alikutana na mtenda miujiza Yesu Kristo kwa kumtumia mtumishi wake Prophet Joseph , na hakika Mungu hakumwacha alimponya na akapokea uzima papo hapo.


                        Akiingia kwenye nyumba ya Mungu tayari kupokea uponyaji wake.
                                       Anavyoonekana katika picha akiwa na magongo.
                                                        Akitembea bila ya magongo.
                                       Magongo yakiwa juu na akitembea mwenyewe.
                                      Akishuhudia matendo makuu ya Mungu.

Kupokea uponyaji kutoka kwa Mungu ni sekunde tu endapo utaamini manabii wake na kazi ambazo Yesu Kristo anatenda hata sasa kupitia wapakwa mafuta wake. Hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu wala hakuna ugonjwa ambao hawezi kuuponya kwake yeye kuna spea zote. Kwa imani tu utafunguliwa kutoka katika kila aina ya kifungo.

                                                 UTUKUFU KWA MUNGU JUU!!!

No comments:

Post a Comment