Felista Ludela alikuwa akivuka barabara katika eneo la Tazara jijini Dar es salaam, lakini wakati akivuka pikipiki ilimgonga na kusababisha mfupa wa mkono wake kuvunjika. Alikwenda hospitali wakamfunga kifaa maalum ili mfupa uweze kuunga. Kwa neema ya Mungu dada Felista aliweza kufika katika nyumba ya Mungu Life in Christ Ministries Zoe, wakati wa kipindi cha kuabudu Yesu Kristo mtenda miujiza alimponya na kuweza kuondoka kifaa hicho katika mkono wake na maumivu yote yalimwacha palepale.
Jinsi alivyoingia kwenye nyumba ya Mungu.
Akionekana ni mwenye maumivu hii ni kabla ya maombi.
Akiondoa kifaa hicho katika mkono wake wakati wa kipindi cha kuabudu.
Akiwa ameondoa kifaa hicho mara baada ya kupokea uponyaji.
Akimshukuru Mungu kwa kumponya.
Akishuhudia jinsi Mungu alivyomponya.
Kifaa hicho kikiwa chini kuonyesha kuwa hakihitaji tena katika maisha yake, na ni ishara kuwa Mungu amemponya kabisa.
UTUKUFU KWA MUNGU!!!
No comments:
Post a Comment