Ritha Swai alifika kwenye nyumba ya Mungu Life in Christ Ministries Zoe kumshukuru Mungu, kabla ya kufika kwenye nyumba ya Mungu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu na pia alikuwa akisumbuliwa na roho chafu ya kifafa. Kwa neema ya Mungu mjomba wake aliweza kumleta kwenye nyumba ya Mungu LCM Zoe ili Yesu Kristo wa Nazareth kwa kumtumia mtumishi wake prophet Joseph aweze kumuweka huru. Hali hii ilimtesa kiasi cha kumfanya ashindwe kufanya vyema katika masomo yake, alipita kwenye mstari wa maombezi na hakika kulingana na imani yake, Yesu Kristo alimponya na kufunguliwa kutoka katika maonezi yote ya ibilisi.
Ritha Swai akiwa mbele tayari kushuhudia.
Akiwa na mjomba wake.
Akimtukuza Mungu kwa kumponya.
SIFA NA UTUKUFU KWA MUNGU MWENYE UWEZO.
No comments:
Post a Comment