Hakuna kifungo ambacho Mungu wetu hawezi kumtoa mtu, hata kama imeshindikana kwa wanadamu lakini kwa Mungu wetu anao uwezo wa kuvunja kila pingu . Deus Njweligo alifika katika nyumba ya Mungu LCM Zoe akiwa kwenye kifungo cha unywaji pombe na uvutaji sigara kwa muda mrefu, alijaribu kw anguvu zake kuacha lakini haikuwezekana. Ndipo alipopata neema ya kujua mahali hapa na yeye kuamua kukimbilia kwa Yesu Kristo wa Nazareth ili amtoe kutoka katika kifungo hicho. Alifika kwenye mstari wa uponyaji na ndipo alipoonyesha shauku yake ya kutaka kutoka katika kifungo cha unywaji pombe na uvutaji sigara. Kwa rehema na neema za Mungu aliwekwa huru na Yesu Kristo wa Nazareth kwa kumtumia mtumishi wake prophet Joseph.
Ndugu Deus Njweligo akiwa kweney mstari wa uponyaji.
Akionyesha shauku ya kutaka kutoka kwenye kifungo hicho.
Prophet Joseph akiifukuza roho chafu ya pombe na uvutaji sigara kwa jina la Yesu Kristo, kutoka kwa ndugu Deus.
Akinywa pombe hiyo kuonyesha ni kweli alikuwa anatumia pombe hiyo.
Mara baada ya kufunguliwa hakuweza kuinywa pombe hiyo tena na ikamfanya aitapike. Utukufu kwa Yesu Kristo wa Nazareti.
No comments:
Post a Comment