TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 28 September 2014

VIFUNGO VYA SIGARA,POMBE VYAONDOLEWA KWA JINA LA YESU KRISTO

Ndugu Rodrick Mtui alikuja akiwa anahitaji msaada kutoka wa Bwana wetu Yesu Kristo,ndugu huyu alikuwa kwenye kifungo cha unywaji wa pombe.

                               Hapa akieleza jinsi kifungo hiki cha ulevi kinavyomtesa.
                                  Akiwa ameshikilia pombe hiyo ijulikanayo kama kiroba
                      Prophet Joseph akiamuru roho chafu ya ulevi kumuacha ndugu yetu.

                                 Akiwa amechukuliwa na nguvu ya Mungu.
                                         Akimshukuru Mungu kwa kuwa huru.


2. Ndugu yetu Elijah Kawala mkenya anayeishi nchini Marekani alifika katika huduma ya Life in Christ Ministries naye akitaka kuwekwa huru na Yesu Kristo mtenda miujiza, kutoka katika kifungo cha uvutaji sigara.


             Prophet Joseph akiamuru kila roho inayosababisha kaka yetu avute sigara imuache huru                                                   kwa jina la Yesu Kristo.

                  Hapa ni baada ya kuwa huru hakuwa na hamu tena ya kuona wala kuvuta sigara tena.

                       Akiwa mwenye furaha na akimshukuru Mungu kwa kumtoa katika kifungo hicho                                  cha uvutaji sigara.

YESU AKISEMA IMEKWISHA IBILISI HAWEZI KUZUIA .SIFA KWA YESU KRISTO WA NAZARETH.




UPONYAJI WAKATI WA MASS DELIVERANCE

Mama huyu alipokea uponyaji wakati wa Mass Deliverance,alikuja akiwa amevaa bandage kwenye mguu wake uliokuwa umeumia na alikuwa na maumivu makali. Lakini wakati wa Mass Deliverance (Kufunguliwa kwa pamoja ) aliweza kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.


                               Mama huyu akishuhudia ambavyo amepokea uponyaji wake.
                                               Akitoa bandage mguuni .

                                       Hivi ndivyo mguu wake unavyoonekana.
                                         Hapa akiupiga kuonyesha kwamba hana maumivu tena.
                       Hapa akikimbia kuonyesha kwamba maumivu yameshamwacha kabisa.
Akiweka bandage kwenye ukuta wa uponyaji ishara ya kwamba maumivu sio sehemu yake tena na ishara ya kwamba hakika Yesu Kristo kamponya kabisa. 

                                                  Jina la Bwana libarikiwe!!!

VIFUNGO VYAKATIKA KWA JINA KUU LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Ibada ya jumapili tarehe 28/9/2014 ilianza kwa nguvu za Mungu kuonekana mahali hapa, Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alipoingia aliungana na Zoe worship team kukaribisha uwepo wa Roho Mtakatifu katika ibada hii na tuliona nguvu za Mungu zikishuka bila ya kizuizi cha aina ya yoyote.


                                          Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph.
                                            Maelfu ya watu wakimuabudu Mungu.
   Kila aina ya vifungo na minyororo ya shetani vikiwaacha watu kwa jina la Yesu Kristo wa    Nazareth.
                                                Mama huyu akitapika kila aina ya sumu.
                                                  Sumu iliyotapikwa na mama huyu .
    Dada huyu naye akitapika,kuonyesha kwamba hata iwe sumu ya aina gani kwa amri ya jina la    Yesu sumu hiyo itatoka.

Roho chafu ikijidhihirisha na kumtoka dada huyu kuonyesha kuwa hakuna roho chafu itakayokaa katika hekalu la Roho Mtakatifu.

Saturday, 27 September 2014

KUKABIDHIWA WATOTO KWA MUNGU.

Jumapili hii ya tarehe 21/9/2014 ilikuwa ni siku maalum ya kuwakabidhi watoto kwa Bwana, Prophet Joseph alieleza kuwa kwenye dini wanabatiza watoto na kusema kuwa ni kinyume na Neno la Mungu, kwasababu watoto wanatakiwa wakabidhiwe kwa Mungu na si kubatizwa.

Kwa Imani watoto wanakabidhiwa kwa Mungu kama Yesu Kristo alivyokabidhiwa kwa Bwana wakati akiwa mtoto na alipofikia umri wa miaka 30 alibatizwa na Mwinjilisti Yohana Mbatizaji.
Luka 2:22 inasema Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa, Joseph na Mariam walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana. 




                                       Wazazi wakiwa na watoto wao.














Sunday, 21 September 2014

APOKEA UPONYAJI WA KITOVU KUTOKA KWA YESU KRISTO

Kaka yetu alikuwa na matatizo yaliyodumu kwenye mwili kwa muda mrefu, hasa kwenye kitovu chake hii ilisababishwa na alipokuwa mdogo wazazi wake kuchukua kitovu chake kwa mambo ya kimila kwasababu wazazi wake ni waabudu mizimu. Lakini alipokutana na Yesu mfungua vifungo aliweza kuwa huru kabisa mbali na kuonewa na ibilisi.

                   Prophet Joseph akiamuru kila roho iliyoshikilia kitovu chake kumwachia.



                            Tunaona roho hiyo chafu ikimwacha kaka huyu.
                                 Baada ya kuwa huru akimshukuru Mungu.


                           Kila roho chafu inasalimu amri kwa jina la Yesu Kristo.

APOKEA UPONYAJI WA KIFUA NA SIKIO

Dada Catherine Mathew alikuja akiwa anasumbuliwa na matatizo ya kifua yaliyopelekea ashindwe kupumua vizuri na pia alikuwa na tatizo la kutokusikia vizuri kwa muda mrefu hakuweza kusikia kitu chochote kwa kutumia sikio hilo, lakini wakati mtumishi wa Mungu Prophet Joseph alipoamuru kila minyororo ya ugonjwa iliyomshikilia mtu imwachie ndipo  dada Catherine aliweza kupokea uponyaji wake wa kifua na sikio hapo hapo.

                    Akieleza jinsi ambavyo alikuwa anasumbuliwa na magonjwa hayo.
Hapa tunaona akiwa ameziba sikio lake la kulia na Prophet Joseph akimwongelesha kwa mbali na yeye alisikia bila ya tatizo lolote,hii ni baada ya maombi.
Hapa akihema bila ya kuwa na matatizo ya kifua tena. Matatizo ya  kifua na sikio yakawa ni historia katika maisha yake.

Ahsante Yesu kwa kuendelea kuwaponya watu wako.

MAUMIVU YA MUDA MREFU YAONDOLEWA NA YESU MTENDA MIUJIZA

Dada Fatma Victor alikuja akiwa na maumuvu  katika upande wa kulia yaliyodumu kwa miaka 3 na alikuwa akihisi mwili wake kuwa ni mzito pia alikuwa akishindwa kujigeuza akiwa kitandani kutokana na maumivu hayo aliyokuwa nayo. Lakini mara baada ya maombi yaliyoongozwa na Prophet Joseph dada huyu alipokea uzima kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.

     Hapa akionyesha jinsi ambavyo anaweza kugeuka bila ya kuwa na maumivu ya aina yoyote.
                     Hapa akijibonyeza kuonyesha kuwa roho ya maumivu imeondolewa.


KUSIFU KUNAWAPASA WANYOFU WA MOYO...

Baadhi wa maelfu waliofika katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe ,wakimwabudu Mungu ,wakiwa wanaongozwa na Zoe Worship Team,huku wakitafakari ukuu na uweza wa Mungu ishara,maajabu na miujiza ilionekana.

Zoe Worship Team.



Sifa na Utukufu ni kwa Mungu aliye juu!!! Mungu wa Ibrahimu,Isaka na Yakobo.

APOKEA UPONYAJI WAKATI WA MAOMBI YA PAMOJA.

Mama yetu Margret kutoka Tabata alikuwa na maumivu katika mguu wake wa kushoto kuanzia alipokuwa na umri wa miaka 14 na alipokwenda hospitalini aliambiwa kuwa ana matatizo ya ugonjwa wa moyo, alikuwa akipata maumivu makali yalipelekea hata ashindwe kugeuka akiwa kitandani na pia alikuwa na maumivu ya bega lakini baada ya maombi yaliyoongozwa na Prophet Joseph kwa kutumia jina la Yesu Kristo alipokea uponyaji na kuwa mzima kabisa...





Sunday, 14 September 2014

UTI WA MGONGO WAKAA SAWA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Dada Irene William alikuja kushuhudia matendo makuu ambayo Mungu alimtendea, alikuja akiwa na tatizo la miguu ambalo lilisababishwa na tatizo la uti wa mgongo, tattizo hili lilisababisha awe na maumivu makali ambayo yalisababisha ashindwe kusimama kwa muda mrefu na kushindwa kutembea kwa muda mrefu,lakini jumapili ya tarehe 24/8/2014 alisoma Yohana 10:10 inayosema  Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Mara alipoamini na kukiri neno hili alipokea uzima wake kutoka kwa Yesu Kristo.
Dada Irene akiwa ameshikilia mkononi lumbar corset au mkanda maalum uliokuwa ukimsaidia wakati akiwa na maumivu.
                Mume wake dada Irene akimshukuru Mungu kwa kumponya mke wake.
                      Dada Irene akiwa na mumewe wakimshukuru Mungu.

Akiiweka Lumbar Corset kwenye ukuta wa uponyaji ikiwa ni ishara kuwa haihitaji tene kuvaa mkanda huo kwa kuwa ameshapokea uponyaji wake.

Hakika Yesu Kristo anaendelea kutenda hata sasa hakusema kuwa hakutakuwa na uponyaji au kufunguliwa La hasha! bado anaponya hata sasa ukiamini tu atakuponya nawe utakuwa mzima kabisa haijalishi ugonjwa au mateso gani unayo akisema imekwisha amini kuwa imekwisha. Ahsante Yesu kristo!!!

MAUMIVU YA SIKIO YAONDOLEWA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Dada Esther Njeri kutoka nchini Kenya alikua akiwa na maumivu katika sikio na pia sikio lililkuwa linatoa usaha ilimbidi kila mara atumie kitambaa kufuta usaha, mara baada ya maombi alipokea uponyaji wake na pia alitoa ushuhuda kuwa alikuja mwaka jana akiwa na tatizo la mimba kutoka kila alipopata ujauzito mimba ilitoka lakini mara baada ya kuja Zoe na kupata maombi ameweza kupata neema ya kupata ujauzito na kujifungua bila ya kuwa na tatizo lolote na alijifungua mtoto aitwaye Imani.


Dada Esther akishuhudia matendo makuu ambayo Mungu amemtendea.
UTUKUFU KWA MUNGU!!!

KUFUNGULIWA KWA PAMOJA (MASS DELIVERANCE)

Kila siku ya ibada tunazidi kumwona Mungu akiwafungua watu na kutenda miujiza mbalimbali, hakika Mungu tunayemtumikia sio wa kawaida. Katika ibada ya jumapili 14/9/2014 Mungu aliwafungua watu mbalimbali kupitia mtumishi wake Prophet Joseph.


Baadhi ya maelfu waliofika ktika huduma ya Life in Christ Ministries Z.oe wakiwa wamechukuliwa na nguvu ya Mungu,nguvu iletayo afya,uzima na kufunguliwa kutoka katika mikono ya ibilisi

Sunday, 7 September 2014

UPONYAJI WAKATI WA PRAYER LINE.

Kila jumapili katika mstari wa uponyaji  (Prayer Line) tumeendelea kuuona ukuu na utukufu wa Mungu kupitia Prophet wake Prophet Joseph,maelu ya watu wamekuwa wakiponywa haijalishi ni ugonjwa wa aina gani, kuna waliokuja na Ukimwi,Kansa,Kisukari,Presha,Ulemavu na magonjwa mengine mengi lakini tumeshuhudia Yesu Kristo akiwaponya na kuwafungua na kuwa huru kabisa.



Kaka yetu Nisamba Aginom kutoka Congo aliweza kupata neema ya unabii kutoka kwa Mungu kupitia Prophet Joseph kuwa kila akienda kuoga mwili wake hutetemeka mara anagusa maji na ndio chanzo cha biashara zake kutokwenda vizuri naye akakiri kuwa ni kweli tupu.
                       Hapa prophet Joseph akimfungua kwa jina la Yesu Kristo.

                                            Akiwa chini kwa nguvu ya Mungu.
           Prophet Joseph akionyesha upendo wa kumfuta kaka yetu mara baada ya kufunguliwa.
                           Hapa Prophet Joseph akimkumbatia kaka yetu ikiwa ni ishara ya upendo.


 Mama yetu Dotto Fabian alikuja na tatizo la mguu, ansema lilianza kama muwasho alikuwa na muwasho kwenye mguu ghafla mguu ukaanza kuvimba na kujaa usaha na akawa hawezi kuembea .
 Kama mguu unavyoonekana hapa, lakini mara baada ya maombezi maumivu yote yakamwacha na akaweza kutembea na kukimbia bila ya kuwa na maumivu.

                                   Hapa akimshukuru Mungu kwa kumponya.

         Ndugu yetu Jige Mafuru alipata ajali ya pikipiki na kusababisha mguu wake kuvunjika mara mbili.


                                     Hapa akionekana mguu ukiwa na vyuma.

Hapa Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akiamuru uzima kuingia katika mguu wa ngugu yetu.
                  Hapa akisimama mara baada ya roho ya ajali na maimivu kumwacha.

                       Hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu. Yanayoshindikana kwa wanadamu kwake yanawezekana.