TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Saturday, 20 December 2014

YESU KRISTO WA NAZARETH ANAENDELEA KUUNGA MIFUPA HATA SASA...

1.Ndugu Mathayo John kutoka Ruvuma alipata ajali ya kugongwa na pikipiki akiwa Songea, na kusababisha kifundo cha mguu kuvunjika vipande alipelekwa hospitali na kuwekewa chuma ili kusaidia mfupa kuunga. Na alipangiwa operesheni nyingine lakini jinsi Mungu alivyo Mkuu na upendo mwingi wakati wa kipindi cha Mass deliverance mtumishi wa Mungu Prophet Joseph aliamuru mifupa iliyovunjika kuunga ndugu yetu alipokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth na maumivu yote yakamwacha na akawea kutembea bila ya msaada wa magongo.


                                   Ndugu Mathayo akiwa na fimbo aliyokuwa akitembelea.
 Prophet Joseph akiamuru mfupa kuunga na roho ya maumivu kumwacha kwa jina la Yesu Kristo.
               Fimbo ikiwa chini mara baada ya kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo.
                                                  Akitembea bila ya msaada wa fimbo.
                                          Akimshukuru Mungu Baba kwa kumponya.
                                 Akishuhudia matendo makuu ya Mungu aliyomtendea, na kuweza kutembea bila ya msaada wa gongo hakika ana kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kumponya, maana gongo si sehemu yake kwa Jina la Yesu Kristo.

2. Rose Didas kutoka Kimara alipata ajali ya basi iliyopelekea mguu wake kuvunjika vibaya,alifanyiwa operesheni na kuwekewa chuma katika mguu wake ili uweze kupona. Alikuwa amelala kwa muda wa miezi miwili huku akisaidiwa kufanya kila kitu. Kwa Neema ya Mungu alipata habari njema kuhusu huduma hii ya Life in Christ Ministries Zoe, hakika Mungu hakumwacha wala hakumsahau katika ibada ya jumapili ya tarehe 14/12/2014 katika kipindi cha mass deliverance, maombi yaliyoongozwa na Prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu aliweza kupokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth.

                  Dada Rose Didas akiwa katika nyumba ya Baba yetu wa Mbinguni.
                                         Mguu unavyoonekana katika picha.

                                      Akitembea bila ya msaada wa gongo wala bendeji.
 Matendo makuu ya Mungu yanaendelea kuonekana hata sasa dada Rose Didas akishuhudia matendo makuu akiwa hana maumivu ya aina yoyote. Sifa na Utukufu kwa Bwana.





No comments:

Post a Comment