TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Sunday, 31 August 2014

PROFESSOR JAY AKIMFURAHIA MUNGU WA ZOE

Mwanamziki wa bongo fleva Joseph Haule au kwa jina la kisanii Professor Jay akimshukuru Mungu kwa kumtoa katika roho ya ulevi na pia anamshukuru Mungu sana kwa maana alikuja katika huduma hii ya Life in Christ Ministries Zoe akiwa na maumivu ya miguu lakini Mungu alimponya kabisa na alisema ana kila sababu ya kuendelea kumshukuru Mungu kwasababu amekuwa kwenye sanaa kwa muda usiopungua miaka 20 lakini hakuwa na mafanikio kama aliyonayo sasa baada ya kumpokea Yesu Kristo wa Nazareth.


Hapa Professor Jay akiwa katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe.

Professor Jay akishuhudia maelfu ya waliofika katika huduma ya LCM jinsi ambavyo Mungu amemtendea.





Professor Jay akimwimbia Mungu katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe... Hakika sanaa bila Mungu haiwezekani.Utukufu na sifa kwa Mungu mwenye uwezo wote.

MUNGU NI MWEMA

Hakuna litakalo endelea kwenye nyumba ya  Mungu Life in Christ Ministries Zoe, bila Mungu kumfunulia Prophet wake,wakati ibada ikiendelea kijana huyu alikutwa na Security akizunguka zunguka katika eneo la kuegesha magari,ndipo mmoja wa security alipomleta ndani ya kanisa, Prophet Joseph akamuuliza baba yake wa mbinguni ndipo akapokea ujumbe kutoka kwa baba wa mbinguni kwamba "Muonyeshe kijana huyu kuwa hii ni nyumba yangu" Prophet Joseph akasema kuwa kijana huyu ana roho ya wizi na hapaswi kulaumiwa kwani adui yetu si mtu bali ni shetani.



Mmoja kati ya masecurity wa LCM Zoe akimwingiza kaka huyu ndani ya kanisa.


Prophet Joseph akimuombea kaka huyu roho chafu ya wizi imuachie." Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa". Luka 6:37.


                         Prophet Joseph akiifukuza roho ya wizi kwa kaka huyu.


Akimshukuru Mungu kwa kumweka huru kutoka katika kifungo cha wizi.

Yohana 10:10,Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. 









YOTE YAWEZEKANA KWAKE YEYE AAMINIYE

Ndugu hawa waliweza kupokea uponyaji wao baada ya Prophet Joseph kusoma neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Zaburi 107:20, "Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao".  Pindi neno hili liliposomwa watu walipokea uponyaji wao na kufunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali. Hawa  ni baadhi ya maelfu waliofika katika huduma ya LIFE IN CHRIST MINISTRIES ZOE na kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth akimtumia mtumishi wake Prophet Joseph.

 Dada Joyce kutokea Mwanza alikuja akiwa na maumivu ya mgongo baada ya kusoma neno hilo alipokea uzima hapo hapo,hapa akimshukuru Mungu kwa kumponya.
Dada Joyce akiwa ameinama kuonyesha kwamba hana tena maumivu ya mgongo.
Dada yetu Amina kutoka Rufiji alikuja akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo na pia alikuwa hawezi kukaa kwenye mkusanyiko wa watu wengi kutokana na ugonjwa huo lakini baada ya kusoma neno hilo la Mungu alipokea uponyaji wake mara moja.

                                Yanayoshindikana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana .

Sunday, 24 August 2014

AFUNGULIWA NA YESU KRISTO KUTOKA KATIKA KIFUNGO CHA USHOGA

Kaka yetu David Don Bosco, aliyekuwa akiitwa Aunt Diana jina alilokuwa akitumia wakati akiwa shoga. Aliteseka na hali hii ya ushoga kwa muda wa miaka 9 hali hii ilimuanza pindi alipomaliza elimu yake ya msingi, pia alipoteza wazazi wake akiwa katika umri mdogo hivyo ilipelekea alipomaliza shule kutafuta kazi ambapo alipata kazi za ndani, ndipo baba mwenye nyumba alipomlazimisha kufanya naye mapenzi kaka David alipokataa baba yule alimlawiti kinguvu.

Alikimbia kutoka Tabora na kuja Dar es salaam ambapo alifikia katika kituo cha kulelea watoto yatima baada ya muda mfupi alitoka kwenye kituo hicho na kuingia mitaani ambako alikutana na kijana ambaye alimuahidi kumsaidia bila kufahamu kuwa ule ulikuwa ni mtego wa ibilisi kwake. Kaka yule alimchukua na kumpeleka nyumbani kwake ambako alikuwa na watoto wengine ambao alikuwa akiwauza kwa wanaume mbalimbali ndipo kaka David alipojikuta ameingia moja kwa moja kwenye hali hii ya ushoga.

Baada ya muda alikutana na mwanaume mwingine ambaye aliamua kufunga naye ndoa na kuishi kama mke na mume,alimbadilisha na kuwa kama mwanamke kabisa,kaka huyo alikuwa akimnunulia nguo za kike na matiti bandia na kisha alimpulizia kemikali katika uume wake na kusababisha uume wake kutokufanya kazi kabisa ili awe kama mwanamke kamili. Baada ya mume wake kufariki dunia katika ajali kaka David alikutana na wakina dada wanne ambao walikuwa wakitengeneza filamu za ngono kaka David akajikuta kwenye mtego mwingine tena wa kuigiza sinema za ngono alikuwa akifanya mapeni na wanaume wawili au watatu kwa wakati mmoja hata ilifikia kufanya mapenzi na mbwa.
Akiwa shoga alikuwa akitembea usiku tu maana aliogopa kutembea mchana akijiogopea manyanyaso aliyokuwa akiyapata kwenye jamii.
Ndipo Prophet Joseph aliposema kuwa atafunguliwa mara mbili, mara ya kwanza nikuondoa ili roho ya ushoga iliyokuwa imemvamia na kufunguliwa kwa pili ni kufunguliwa kutoka katika roho ya mbwa ambayo imemfanya afanye mapenzi na wanyama kama mbwa.


                                         Akieleza kwa machozi hali hii ilivyomtesa.


                                        Prophet Joseph akikemea roho ya ushoga imwache kaka David.
                                            Roho hiyo chafu ikijidhihirisha ndani yake.

 Prophet Joseph akiamuru uume wa kaka David kurudi kama ambavyo Mungu baba alimuumba,hapa tunaona nguvu ya Mungu ikirudisha nguvu hiyo.Kutokana na nguvu ya Mungu kila kilichokufa chaweza kurejeshewa nguvu tena.


                                            Akiwa mwenye furaha tele baada ya kufunguliwa.
           Kaka yetu David akiwa anaonekana mwenye furaha baada ya kufunguliwa na kuwa huru kabisa.

 Mtumishi wa Mungu Prophet Joseph akicheza kwa furaha na kaka David baada ya kaka David kuwekwa huru.
                           Akimpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.


Maelfu waliofika Life in Christ Ministries Zoe wakimshukuru Mungu kwa kumfungua kaka yetu kutoka katika kifungo cha ushoga. Kwa Mungu hakuna linaloshindikana!!!

Luka 15 :24 inasema ;
Kwa sababu huyu mwanangu alikuwa amekufa, kumbe yu mzima alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana.` Wakaanza kufanya sherehe.




WAPOKEA UPONYAJI WA MACHO KUTOKA KWA YESU KRISTO MPONYAJI

Dada huyu kutoka Tanga alikuwa akisumbuliwa na macho kwa muda mrefu, ilipelekea hata kushindwa kutazama jua kila alipotazama jua alipatwa na hali ya kizunguzungu ikasababisha aanze kutumia miwani alipofika katika huduma ya LIFE IN CHRIST MINISTRIES ZOE Yesu mponyaji alimponya na kuwa mazima kabisa.

                                                    Hapa akieleza hali aliyokuwa nayo.
Akiiweka miwani katika ukuta huu wa uponyaji ikionyesha kuwa ameshapokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo mponyaji. Utukufu kwa Mungu mwenye uweza wote!!!


Dada huyu pia naye alipokea uponyaji wa macho ambapo alikuwa hawezi kutazama jua au mwanga mkali,Prophet Joseph alimwita na kumuuliza kwanini anavaa miwani,ndipo Prophet Joseph akamwambia kuwa ameshapokea uponyaji wake haitaji tene kuvaa miwani.


                                                 Akiangalia jua bila ya kutumia miwani...
                                     Akimshukuru Mungu kwa kumponya macho.

                                         UTUKUFU KWA MUNGU MWENYE UWEZA WOTE.!!!

Sunday, 17 August 2014

AFUNGULIWA KUTOKA KATIKA KIFUNGO CHA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA

Hakika hakuna linaloshindikana kwa Mungu kaka yetu Claude alikuwa ameathirika na utumiaji wa madawa ya kulevya kwa muda wa miaka mingi na yeye kama yeye hakuweza kujitoa katika gereza hili kwa miaka yote hii, hali hii ilimtokea alipokuwa nchini Zambia kutokana na ushawishi wa marafiki akajikuta ameanza kutumia madawa ya kulevya aina ya Heroin. Aliporudi nchini Tanzania alishindwa kuacha kwahiyo ilimbidi aendelee kutumia. Kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho, ndipo alipoamua kuja katika huduma ya Life in Christ Ministries Zoe kwa ajili ya kufunguliwa na Yesu Kristo wa Nazareth akimtumia mtumishi wake Prophet Joseph.


 Kutokana na utumiaji wa madawa ya kulevya hakuwa anaweza kupata usingizi ndipo Prophet Joseph alipoamuru aweze kupata usingizi kama tunavyoona kwenye picha hii akiwa amelala usingizi.
Akimshukuru Mungu kwa kumfungua kutoka katika kifungo cha utumiaji wa madawa ya kulevya.
SIFA NA UTUKUFU KWA MUNGU ALIYE JUU!!

MUNGU WETU ANAENDELEA KUTENDA HATA SASA

Ibada imekwisha kuanza katika nyumba ya Mungu, LIFE IN CHRIST MINISTRIES.  Kwahiyo ni vema tukaanza pamoja Prophet Joseph ameingia na kuanza kusoma Mwanzo 18:14 ambayo inasema" kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA?" Pindi aliposoma tu neno hili  tumeona nguvu ya Mungu ilianza kuponya watu na kuwafungua watu mbalimbali, kuna watu waliofika wakiwa hawawezi kutembea lakini kutokana na kuamini neno la Prophet ambaye ametumwa na Mungu mwenyewe, watu walipokea uponyaji hapohapo, hakika Mungu wetu anaendelea kutenda na ni mshindi na hajawahi kushindwa hata siku moja.... HALELUYA KWA BWANA.

                           Watu waliokuwa wamechukuliwa na nguvu ya Mungu.


       Ndugu aliyekuwa hawezi kutembea akiwa anatembea baada ya kuamini neno la Mungu liliongozwa na Prophet Joseph.
                                  Mama huyu akiwa ameweza kutembea kwa nguvu ya neno la Mungu.

                                 Mama huyu akiwa ameweza kutembea bila ya kutumia fimbo.
 Kaka huyu aliyekuwa na maumivu makali ya mguu kwa miaka 3 baada ya kusikia neno la Mungu akawa mzima na kuweza kutembea.






Sunday, 10 August 2014

PROPHET JOSEPH AONGOZA MAELFU KUIOMBEA TANZANIA

Prophet Joseph akiongoza maelfu waliofika katika ibada alisema ni muhimu sana kuliombea taifa letu pamoja na viongozi wake. Alisema kuwa kuna sababu ya sisi kuzaliwa katika taifa hili.

                                    Prophet Joseph akiwa ameshikilia bendera ya Tanzania.

 Nyuma wainjilisti na mashemasi wakiwa na bendera ya taifa la Tanzania tayari kwa kuliombea taifa la Tanzania.

TOTAL DELIVERANCE

Hakuna kifungo ambacho Yesu hawezi kukifungua wala hakuna ngome Yesu asiyoweza kuivunja. Kaka David alikuwa kwenye kifungo cha ulevi  wa bia ya Castle light kwa muda mrefu ndipo alipoamua kwamba lazima ulevi huu ufikie mwisho wake lakini si kwa nguvu zake maana kwa nguvu zake alikwisha shindwa kuacha ndipo alipoamua kutafuta mahali ambapo Yesu mtenda miujiza atamfungua, alifika kwenye huduma ya LIFE IN CHRIST MINISTRIES ZOE,na Yesu hakumpita alimfungua naye akawa huru kweli kweli. Kama anavyoonekana kwenye picha. Alikuja na pombe hii ili kuonyesha kwamba ni kweli amekuwa akiitumia pombe hii.
Kaka David akielezea huku akiwa ameshikilia pombe hiyo mkononi.

Prophet Of God Prophet Joseph akimuombea ili kuondoa kiu yote ya pombe iliyomtesa kwa miaka mingi.




Sunday, 3 August 2014

MATESO YA MIAKA MINGI YASALIMU AMRI KWA JINA LIPITALO MAJINA YOTE JINA LA YESU KRISTO

Dada Doreen aliteseka kwa miaka mingi katika kifungo cha ulevi,kupiga punyeto, na kifungo cha usagaji.Hii ilitokea alipokuwa mdogo akicheza na watoto wenzake mara katika kundi alilokuwamo kulikuwa na mtoto wa kike ambaye alimzidi umri, mara wakiwa wanacheza binti huyo alianza kumtomasa tomasa dada Doreen, na yeye bila kuelewa aliona ni jambo la kawaida tu. Mara alipofika umri wa kujitambua alijikuta akiwachukia wavulana na kupendelea kuwa na uhusiano na wasichana wenzake.Ndipo siku moja kutokana na kuwepo kwenye kifungo cha ulevi wa kupindukia alikutana na dada mmoja pamoja na mumewe, walikunywa sana ilipofika usiku wakamwambia akalale nyumbani kwao, dada Doreen alipokubali akashangaa kuwa wote watatu wanalala chumba kimoja,alipouliza wakasema hakuna tabu.Wakati wamelala akashangaa kuona mume wa yule dada akimpapasa, alimkatalia lakini yule dada alikuwa hajala akmwambia amkubalie ni jambo la kawaida tu, akaanza kusagana na yule dada kisha yule kaka akawaingilia wote. Mateso haya na vifungo hivi vilimtesa mpaka alipoamua kufika katika huduma ya LIFE IN CHRIST MINISTRIES ZOE ili afunguliwe na Yesu Kristo mtenda miujiza. Alifika na akawekwa huru kabisa.

                        Dada Doreen akielezea ni kwa jinsi gani ameteseka na vifungo hivi.
                          Prophet Joseph akiamuru roho hizo chafu kumwachia dada Doreen.
            Maelfu ya waliofika wakishangilia baada ya dada Doreen kuwekwa huru, Hakika kuwekwa huru kwa mwingine ni furaha yetu sote.