TEACHING,HEALING,PROPHECY & DELIVERANCE

.

Wednesday, 2 September 2015

KANSA NA FIBROID YAKOMA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Julieth Ngemela aliletwa kwenye nyumba ya Mungu akiwa mdhaifu sana kutokana na kusumbuliwa na tatizo la kansa lakini mbali na kusumbuliwa na kansa pia alikuwa akisumbuliwa na uvimbe kwenye tumbo (fibroid). Kutokana na uonevu wote huo wa ibilisi hakuweza kutembea wala kukaa aliletwa kwenye nyumba ya Mungu L.C.M Zoe na kulazwa kwenye machela kutokana na kushindwa kukaa.

Wakati wake wa kupokea uponyaji kutoka kwa mtenda miujiza Yesu Kristo wa Nazareth ulifika, wakati wa kipindi cha mstari wa uponyaji kilipofika mtumishi wa Mungu prophet Joseph akiongozwa na Roho Mtakatifu alimwekea mkono na papo hapo ndugu Julieth alipokea uponyaji na akaweza kusimama na kutembea kuonyesha kuwa hakika Yesu Kristo wa Nazareth amemponya moja kwa moja na ndio ukawa mwisho wa kansa kumtesa.

                         Ndugu Julieth Ngemela akiwa amejipumzisha kwenye mkeka.

               Akiwa amebebwa kwenye machela tayari kuwekwa kwenye mstari wa uponyaji.
                           Akiwa amewekwa kwenye machela katika mstari wa uponyaji.



                        Prophet Joseph akiamuru roho zote za maumivu kumwacha.
                                Akiamuru udhaifu katika miguu kumwacha.
                                      Prophet Joseph akimwamuru kusimama na kutembea.
                     Mara baada ya maombi alisimama na kutembea mwenyewe bila ya kubebwa.
                                                       Akimshukuru Mungu kwa kumponya.

Friday, 28 August 2015

TATIZO LA MIFUPA LAMWACHA MARA BAADA YA MAOMBI

Mama Elizabeth Joseph alifika katika nyumba ya Mungu Life in Christ Ministries Zoe akisumbuliwa na tatizo la mifupa, tatizo hilo lilisababisha ashindwe kutembea vyema lakini pia hakuweza kukunja miguu yake na pia alikuwa na maumivu makali katika miguu yake na katika mgongo wake.
Alikwenda hospitali vipimo vikaonyesha sehemu ya mifupa yake ilikuwa ikisagika ndipo alipoamua kufika katika nyumba ya Mungu ili aweze kupokea uponyaji kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth, hakika yanayoshindikana kwa wanadamu kwa Mungu yanawezekana. Ulifika wakati wa Yesu Kristo kumponya kupitia mtumishi wake prophet Joseph, wakati wa ibada ya kufunguliwa kwa pamoja mtumishi wa Mungu pophet Joseph aliamuru kila aliye mgonjwa aweze kupokea uponyaji ndipo ndugu yetu Elizabeth Joseph aliweza kupokea uponyaji wake kutoka kwa Yesu Kristo wa Nazareth. Alisimama papo hapo na kuanza kutembea hii ni ikiwa mara ya kwanza kutembea bila ya kushikiliwa baada ya kukaa muda mrefu ya bila kutembea sawasawa.
Mume wake alistaajabu kuona jambo ambalo Mungu amemtendea mkewe alikwenda kwenye madhabahu kushuhudia matendo makuu ya Mungu. 


                              Dada Elizabeth akiwa anaingia kwenye nyumba ya Mungu L.C.M Zoe.

                 Akiwa kwenye nyumba ya Mungu tayari kwa kupokea uponyaji wake.
               Hapa akisaidiwa kusimama na mtenda kazi katika ya nyumba ya Mungu.
                 Akitembea mwenyewe bila ya msaada wa mtu yeyote hii ni baada ya maombi.
                                     Akishuhudia matendo makuu ya Mungu.
                                   Mume akimshukuru Mungu kwa uponyaji wa mke wake.
                                                              Akitembea bila ya tatizo lolote.

Yanayoshindikana kwa madaktari kwa Yesu Kristo wa Nazareth yanawezekana. Utukufu kwa Mungu.


Monday, 10 August 2015

ROHO YA USHOGA YAMWACHA HURU KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH

Francis Moses amekuwa katika kifungo cha ushoga yapata miaka 9. Mama yake kwa upendo mkuu aliweza kumleta katika huduma ya Life in christ Ministries Zoe ili Bwana wetu Yesu Kristo aweze kumweka huru. Akiwa na umri wa miaka mitatu nduguzake waliamua kumchukua kutoka Dar es salaam na kwenda kuishi naye jijini Mbeya hii ni kutokana na kwamba mama yake mzazi hakuweza kumlea mara baada ya baba mzazi kufariki dunia.
Ndipo alipokuwa darasa la tatu alikwenda kuoga mtoni akiwa na kijana aliyemzidi umri, walipoanza kuoga yule kijana alianza kumshika mwili wake na ndipo alipomwingilia kinyume na maumbile bila ridhaa ya ndugu Francis. Tokea siku ile aliendelea na mchezo huo, ikafikia hatua ya kutokuweza kujizuia na kuendelea na mchezo huo wa kuingiliwa kinyume na  maumbile na wanaume tofauti tofauti. Akawa akivaa nguo za kike na hata kubadili mwondoko wake na kuwa kama mwanamke ilihali ni mwanaume. Wakati akiwa katika hali hiyo ya ushoga wanaume waliokuwa wakimwingilia walikuwa wakivunja uume wake ili usiweze kufanya kazi sawasawa, amekuwa katika hali hiyo kwa miaka 9. Pia alikuwa katika kifungo cha unywaji pombe na uvutaji ugoro. Kwa neema na upendo wa Mungu, prophet Joseph kwa kutumia jina la YESU Kristo aliweza kumfungua ndugu Francis kutoka katika kifungo hicho cha ushoga.

                                               Ndugu Francis katika picha.

                                            KABLA YA KUWEKWA HURU

                                          Hapa akionekana na suruali ya kike.
                                                  Akiwa na mama yake mzazi.
                                         Akielezea jinsi alivyojikuta katika hali hiyo.


                                               WAKATI WA KUFUNGULIWA
                  Prophet Joseph akiifukuza roho ya ushoga kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
                                       Roho chafu ya ushoga ikijidhihirisha.

                          Prophet Joseph akiamuru uume wa ndugu Francis urudi kuwa sawa.

                   Familia ya wana Zoe wakimtukuza Mungu kwa kumweka ndugu Francis huru.

                                       MARA BAADA YA KUWEKWA HURU
 Hivi ndivyo anavyoonekana baada ya kuwa huru kutoka katika roho chafu ya ushoga.
                                           Akiwa nadhifu na mavazi ya kiume.

                              WIKI MOJA BAADA YA KUWEKWA HURU.

Wiki moja baada ya kuwekwa huru alifika katika nyumba ya Mungu kumshukuru Mungu kwa kumtoa katika roho chafu ya ushoga. 

Katika Wagalatia 5:16-18 inasema; " basi nasema enendeni kwa Roho wala hamtatimiza kamwe tamaa za mwili. 17. Kwasababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. 18. Lakini mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria.

                   Hakika yatupasa kuenenda katika roho ili adui asitutege.

                                                    UTUKUFU KWA BWANA.

Sunday, 2 August 2015

MUNGU WA ZOE AENDELEA KUIFUKUZA KANSA

Leornard Kasanga alifika katika nyumba ya Mungu, Zoe L.C.M akisumbuliwa na kansa ya ini kutokana na kuugua kansa hiyo tumbo lake lilijaa sana, hakuweza kutembea na kula na ilipelekea kuwa dhaifu sana. Alipofika kwenye nyumba ya Mungu hakuweza kukaa ilibidi apumzishwe kwenye sehemu maalum. Prophet Joseph ndipo alipomuita Mungu mponyaji ili aweze kumponya kaka yetu, kwa neema ya Mungu na rehema za Mungu ndugu yetu aliweza kupokea uponyaji wake na papo hapo akasimama na kutembea bila ya kushikiliwa.

                                     Ndugu Leornard akiwa kwenye machela.
                                                       Akiwa ameshikilia tumbo lake.
                                          Aliweza kusimama mara baada ya maombi.
                                          Akitembea bila ya msaada wa mtu mwingine.
                            Akiwa amejitwika machela baada tu ya kupokea uponyaji wake.
                                               Akimtukuza Mungu kwa kumponya.
                               Akishuhudia yale matendo makuu ya Mungu aliyomtendea.
                                                    Akionekana mwenye furaha.
Hakika hii ni kuonyesha kuwa Mungu ni mkuu, aliweza hata kukimbia baada ya kutokuweza kwa muda mrefu.

                                   YESU NI YEYE YULE JANA NA HATA MILELE.
                                             SIFA NA UTUKUFU KWA BWANA.

Sunday, 19 July 2015

KIFUNGO CHA POMBE NA SIGARA CHAONDOLEWA KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI

Hakuna kifungo ambacho Mungu wetu hawezi kumtoa mtu, hata kama imeshindikana kwa wanadamu lakini kwa Mungu wetu anao uwezo wa kuvunja kila pingu . Deus Njweligo alifika katika nyumba ya Mungu LCM Zoe akiwa kwenye kifungo cha unywaji pombe na uvutaji sigara kwa muda mrefu, alijaribu kw anguvu zake kuacha lakini haikuwezekana. Ndipo alipopata neema ya kujua mahali hapa na yeye kuamua kukimbilia kwa Yesu Kristo wa Nazareth ili amtoe kutoka katika kifungo hicho. Alifika kwenye mstari wa uponyaji na ndipo alipoonyesha shauku yake ya kutaka kutoka katika kifungo cha unywaji pombe na uvutaji sigara. Kwa rehema na neema za Mungu aliwekwa huru na Yesu Kristo wa Nazareth kwa kumtumia mtumishi wake prophet Joseph.

                                   Ndugu Deus Njweligo akiwa kweney mstari wa uponyaji.
                         Akionyesha shauku ya kutaka kutoka kwenye kifungo hicho.
 Prophet Joseph akiifukuza roho chafu ya pombe na uvutaji sigara kwa jina la Yesu Kristo, kutoka kwa ndugu Deus.
                     Akinywa pombe hiyo kuonyesha ni kweli alikuwa anatumia pombe hiyo.
     Mara baada ya kufunguliwa hakuweza kuinywa pombe hiyo tena na ikamfanya aitapike.                                                       Utukufu kwa Yesu Kristo wa Nazareti.

Sunday, 12 July 2015

KIFAFA CHASALIMU AMRI KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI

Ritha Swai alifika kwenye nyumba ya Mungu Life in Christ Ministries Zoe kumshukuru Mungu, kabla ya kufika kwenye nyumba ya Mungu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu na pia alikuwa akisumbuliwa na roho chafu ya kifafa. Kwa neema ya Mungu mjomba wake aliweza kumleta kwenye nyumba ya Mungu LCM Zoe ili Yesu Kristo wa Nazareth kwa kumtumia mtumishi wake prophet Joseph aweze kumuweka huru. Hali hii ilimtesa kiasi cha kumfanya ashindwe kufanya vyema katika masomo yake, alipita kwenye mstari wa maombezi na hakika kulingana na imani yake, Yesu Kristo alimponya na kufunguliwa kutoka katika maonezi yote ya ibilisi.

                                          Ritha Swai akiwa mbele tayari kushuhudia.
                                                       Akiwa na mjomba wake.

                                            Akimtukuza Mungu kwa kumponya.

                              SIFA NA UTUKUFU KWA MUNGU MWENYE UWEZO.


Sunday, 28 June 2015

ZOE!!! OUR SERVICE HAS JUST STARTED HERE AT LIFE IN CHRIST MINISTRIES HEAD QUARTERS AT TABATA SEGEREA. WE ARE ALSO BROADCASTED LIVE ON UHURU FM. RADIO 95.7 FM DAR ES SALAAM OR www.uhurufm,co,tz. JUST TUNE THERE AND BE BLESSED AS YOU LISTEN LIVE SERVICE.

Saturday, 20 June 2015

MAUMIVU YA NYONGA YA MUDA MREFU YASALIMU AMRI KWA JINA LA YESU KRISTO

Elisa Kamugisha alikuwa na maumivu ya nyonga ya kulia kwa muda wa miaka 23 na kumsababishia maumivu makali na kutembelea magongo, alikwenda kwenye hospitali mbalimbali ndani na mwisho akapewa rufaa ya kwenda kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi, alifanyiwa uchunguzi mara 5 na ndipo madaktari walipomweleza kuwa kuna viashiria vya kansa katika mwili wake kama hiyo haikutosha akaamua kwenda kwenye hospitali ya wamarekani iliyopo nchini Tanzania na kuamua kwenda kufanya vipimo. Walimfanyia vipimo na kubaini kuwa ana tatizo katika figo zake wakamwandikia dawa na akawa akitumia dawa hizo lakini hazikusaidia.Alipojaribu kila aliloweza kwa uwezo wake na kushindwa ndipo alipoamua kumtafuta Daktari wa madaktari, Yesu Kristo wa Nazareth. Alipofika katika nyumba ya Mungu LCM Zoe alikutana na mtenda miujiza Yesu Kristo kwa kumtumia mtumishi wake Prophet Joseph , na hakika Mungu hakumwacha alimponya na akapokea uzima papo hapo.


                        Akiingia kwenye nyumba ya Mungu tayari kupokea uponyaji wake.
                                       Anavyoonekana katika picha akiwa na magongo.
                                                        Akitembea bila ya magongo.
                                       Magongo yakiwa juu na akitembea mwenyewe.
                                      Akishuhudia matendo makuu ya Mungu.

Kupokea uponyaji kutoka kwa Mungu ni sekunde tu endapo utaamini manabii wake na kazi ambazo Yesu Kristo anatenda hata sasa kupitia wapakwa mafuta wake. Hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu wala hakuna ugonjwa ambao hawezi kuuponya kwake yeye kuna spea zote. Kwa imani tu utafunguliwa kutoka katika kila aina ya kifungo.

                                                 UTUKUFU KWA MUNGU JUU!!!