Julieth Ngemela aliletwa kwenye
nyumba ya Mungu akiwa mdhaifu sana kutokana na kusumbuliwa na tatizo la kansa
lakini mbali na kusumbuliwa na kansa pia alikuwa akisumbuliwa na uvimbe kwenye
tumbo (fibroid). Kutokana na uonevu wote huo wa ibilisi hakuweza kutembea wala
kukaa aliletwa kwenye nyumba ya Mungu L.C.M Zoe na kulazwa kwenye machela
kutokana na kushindwa kukaa.
Wakati wake wa kupokea uponyaji
kutoka kwa mtenda miujiza Yesu Kristo wa Nazareth ulifika, wakati wa kipindi
cha mstari wa uponyaji kilipofika mtumishi wa Mungu prophet Joseph akiongozwa
na Roho Mtakatifu alimwekea mkono na papo hapo ndugu Julieth alipokea uponyaji
na akaweza kusimama na kutembea kuonyesha kuwa hakika Yesu Kristo wa Nazareth
amemponya moja kwa moja na ndio ukawa mwisho wa kansa kumtesa.
Ndugu Julieth Ngemela akiwa amejipumzisha kwenye mkeka.
Akiwa amewekwa kwenye machela katika mstari wa uponyaji.
Prophet Joseph akiamuru roho zote za maumivu kumwacha.
Akiamuru udhaifu katika miguu kumwacha.
Prophet Joseph akimwamuru kusimama na kutembea.
Mara baada ya maombi alisimama na kutembea mwenyewe bila ya kubebwa.
Akimshukuru Mungu kwa kumponya.